Header ads

Header ads
» » Microsoft Waja na Program (App) Matata ya Kukuamsha Asubuhi

 New alarm clock app needs a selfie to stop it going off
Microsoft wamekuja na apps kadhaa kwa ajili ya android na sasa wamekuja na app ya kengere (alarm), Mimicker Alarm, isiyonyamaza hadi ufanye mambo kadhaa. Kuna apps nyingi sana za alarm kwa ajili ya watu wenye usingizi mzito, yaani wagumu kuamka. 

 Kupitia programu yao ifahamikayo kwa jina la Garage ndio wazo na utengenezaji wa app hiyo ulikuja. Zoezi la kusoma (kutamka) sentensi kwa umakini bila kukosea App hii itahakikisha unaaamka kupitia wewe kushiriki katika uchezaji wa gemu. Unaweza kuchagua aina ya mchezo unaotaka kucheza wakati wa kuamka wakati unapoweka alarm. Michezo hiyo ni pamoja na; Kuonesha kitu na wewe kutakiwa kupiga picha kitu chochote karibu yako chenye rangi kama hiyo. 

App hiyo kupitia teknolojia ya utambuaji itatambua kama rangi hiyo ni sahihi, na kama si sahihi basi alarm hiyo itaendelea kuita. Piga picha ya selfie . Chaguo lingine litakuwa ni kukuitaji wewe kupiga picha ya selfie katika ‘pozi’ flani, mfano tabasamu n.k ‘Tongue twister’ 

– utapewa sentensi ngumu kidogo kutamka na utatakiwa kuzitamka kwa usahihi. Ukiamshwa na app ya Mimicker utakutana na zoezi tamu la kuhakikisha umeamka kweli kweli Mpangilio (setting) wa nyongeza ni pamoja na kuchagua ata baada ya kupitia zoezi (mchezo) lolote hapo juu lazima utume matokeo yake kwa marafiki kupitia mitandao ya kijamii na kama utafanya hivyo alarm itaita tena kama kawaida. Kwa sasa app hiyo inapatikana kwa watumiaji wa Android, app nzima inachukua takribani MB 21 na inaweza kupakuliwa kwa simu zenye Android 4.1 KitKat na kuendelea . Toleo la iOS lipo njiani.


Source;; tMetro News
 
>>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post