Satalaiti hiyo ni mojawapo ya sehemu ya Facebook ya Internet.org na itatumika hasa katika upatikano wa mtandao kwa simu za mkononi,tayari shughuli za ujenzi wa satalaiti hiyo unaendelea na uinduzi unatarajiwa kufanyika mwaka 2016.
Mkurugenzi mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg alifahamisha kwamba satalati hiyo inayojulikana kwa jina AMOS-6,itafikisha huduma zake magharibi,mashariki na kusini mwa Afrika.
Facebook ina watumiaji milioni 20 kutoka nchi za masoko makuu kutoka Afrika;Nigeria na Kenya na takwimu zaonyesha kuwa wengi wa watumiaji hutumia simu za rununu.
Aidha kampuni hiyo ilifungua ofisi yake ya kwanza Afrika jijini Johannesburg mnamo mwezi Juni mwaka huu.