Msemaji wa Japan ambaye pia ni mtengezaji wa magari hakutaka kutoa maelezo zaidi kuhusu uwezo wa gari hilo kabla ya wiki ijayo ambapo kutakuwa na na hafla ya maonyesho ya magari jijini Tokyo.
Hata hivyo watengezaji magari wana hofu ya kupata shinikizo kuu kutoka kampuni ya Google iliyo na mpango wa kutengeneza gari lisilohitaji dereva na pia Apple inayozidi kujiendeleza kiteknolojia kwa kufanya utafiti wa kutengeneza gari lakujiendesha.