Timu ya Yanga SC jana imekamilisha kujifua kwa mazoezi makali kwa ajili
ya maandalizi ya kumvaa mnyama Simba siku ya Jumapili tarehe 8 Machi mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Yanga walitoka Botswana na kuunganisha moja kwa moja mjini Bagayomo ambapo wamefikia kwenye Hoteli ya Kiromo View iyopo nje kidogo ya mji wa Bagamoyo.
Jana asubuhi, timu ya Yanga ilifanya mazoezi kwenye uwanja wa Mwanakalenge uliopo bagamoyo mji uwanja ambao hutumiwa mara nyingi na timu hiyo pindi inapopiga kambi mjini humo.
Lakini jioni timu hiyo ilibadili uwanja na kwenda kufanyia mazoezi yake kwenye uwanja wa chuo cha uvuvi Mbegani. Wachezaji walianza kwa mazoezi mepesi lakini kadri muda ulivyokua uanasonga mbele mwali wa timu hiyo Hans van Pluijm alibadili mazoezi na kuongeza kuwa magumu.
Baadaye kikosi cha Yanga kilifanya mazoezi ya kucheza mpira ambapo mwalimu wa timu alisisitiza wachezaji kupasiana pasi za haraka haraka na kuzuia wacheza kukaa na mpira kwa muda mrefu.
Mazoezi ya Yanga yalikusanya umati mkubwa wa wakazi wa eneo la Mbegani na maeneo mengine ya jiran waliofurika kushuhudia mazoezi ya vijana wa Jangwani.
Yanga watakuna na Simba kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara Machi 8 kwenye uwanja wa Taifa, Simba wao wameweka kambi visiwani Zanzibar kujinoa kwa ajili ya mtanange huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka nchini. Timu hio mara ya mwisho kukutana ilikua ni Disemba mwaka jana kwenye mchezo wa ‘Nani Mtani Jembe’ na Simba ikaibuka na ushindi wa goli 2-0.

Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi jana jioni kwenye uwanja wa Mbegani, Bagamoyo
picha na Abdallah Magana
Usisahau kuhungana nami FACEBOOK , TWITTER, INSTAGRAM