Header ads

Header ads
» » VIJANA WALIOTEMBEA KWA MIGUU TOKA GEITA ADI DAR WADHAMINIWA

 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema kuwa vijana watatu waliotoka Geita kuja jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kumuona Rais na kukaidi amri ya kusitisha safari yao, wako nje kwa dhamana.
Kauli ya Wambura inatokana na vijana watatu kutembea kwa miguu kutoka mkoani Geita kwa lengo la kufika Ikulu kuona na Rais na kumweleza kero zao, ambao walikamatwa baada ya kukaidi amri ya kusitisha safari hiyo.
Wambura Alisema kinachofuata sasa ni taratibu za kisheria ikiwamo kufanyika kwa upelelezi na ukikamilika watawasiliana na Mwanasheria wa Serikali kufahamu hatua gani inafuata.
Katibu Mkuu wa Chadema  Dk Willibrod Slaa, alithibitisha kuwa mawakili wa Chama hicho walikwenda kuwatoa vijana hao kwa maandishi na wamechukua jukumu la kuwasimamia mahakamani iwapo watashtakiwa.
Alisema haoni sababu ya vijana hao kukamatwa au kushtakiwa kwa sababu walikuwa wanafanya wajibu wao, kama unampa mtu dhamana ya kukuongoza una haki ya kuhoji endapo hakuongozi vyema na hilo ndilo lengo la vijana hao kutaka kufikisha malalamiko yao kwa Rais.
“Wakishtakiwa mawakili wetu ambao waliwatoa jana ndiyo watasimama mahakamani na tumewadhamini jana wameshatoka, ” alisema Dk Slaa.
Akizungumza na gazeti hili Khalid Selemani ambaye ndiye kiongozi wa msafara huo alisema kuwa walitolewa juzi saa moja na nusu jioni.
Alisema chama kimeamua kuchukua jukumu la kuhakikisha ndoto zao zinatimia kwa kufuata taratibu zote, hivyo wao wanakisubiri chama kiwaandalie utaratibu wa kufika Ikulu.
“Tupo salama mikononi mwa Chadema ambao wamesema jukumu hilo tuwaachie na tumekubaliana hivyo, taratibu zifuatwe ili ikiwezekana kama tunavyoomba tuonane na Rais,” alisema Khalid.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post