Jumuiya ya Afrika Mashariki inafanya mazungumzo kuhusu kupanua mtandao wa simu wa pamoja kwa nchi zote wanachama.
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano ya Kenya Bw. Francis Wangusi amesema kwa sasa Uganda, Rwanda na Sudan Kusini zimeungana kwenye mtandao huo, na sasa wanazumgumza na Tanzania na Burundi kujiunga na mtandao huo.
Kama kupanuliwa kwa
mtandao huo kukifanikiwa, kutapunguza gharama ya kupiga simu ndani ya
kanda hiyo na kutasaidia mchakato wa kuhimiza umoja wa kikanda.
Ameongeza kuwa Tanzania na Burundi ziko tayari kurekebisha sheria zao, ili kujiunga na mtandao huo na kuwanufaisha watu wao.
Ameongeza kuwa Tanzania na Burundi ziko tayari kurekebisha sheria zao, ili kujiunga na mtandao huo na kuwanufaisha watu wao.