Tanzania inatarajiwa kuandaa maonesho ya wazi ya kilimo yatakayofanyika Januari 26 na 27 mwakani katika mji wa Arusha.
Maonesho hayo yanayojulikana kama "Maonesho ya teknolojia ya kilimo ya Tanzania" yatawaleta pamoja wakulima, maofisa, mashirika ya kilimo, mashirika yasiyo ya kiserikali, watafiti, wafanya biashara, pamoja na wawekezaji na wanabenki.
Akiongea kuhusu maonesho hayo, mshauri wa mambo ya sera katika wizara ya Kilimo, mifugo na uvuvi David Nyange amesema teknolojia zitakazoonyeshwa zina uwezo wa kubeba jukumu kubwa kuelekea kilimo cha kibiashara.
Maonesho hayo ya wazi yalianzia katika kituo cha kilimo cha Chisamba nchini Zambia miaka mitatu iliyopita, na yametoa msukumo mkubwa katika sekta ya kilimo nchini humo