Kundi la Yamoto Band
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Nyumbani Kwanza, Mossy Magere, alisema kuwa katika mchezo huo kutakua na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoka kwa Yamoto Band.
Alisema kuwa wasanii hao wanatarajiwa kutoa burudani ya aina yake kwa mashabiki wa mpira watakaojitokeza kwa ajili ya kuchangia fedha za kujenga kituo cha watu wanaoishi katika mazingira magumu ikiwa ni pamoja na walemavu wa ngozi (albino).
“Bendi ya Yamoto ndio inatarajia kutoa burudani ya aina yake katika mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa ambao utatanguliwa na mchezo wa mashabiki wa Yanga dhidi ya Manchester United,” alisema.
