Tovuti ya Gazeti la Maumbile la Uingereza imetangaza wanasayansi 10 muhimu zaidi duniani wa mwaka huu, ambao wote wametoa mchango katika shughuli muhimu za sayansi.
1. Prof. Gabriela Gonzalez
Msemaji wa kikundi cha mradi wa LIGO ametoa mchango mkubwa kwa uchunguzi wa mawimbi ya mvuto na kuthibitisha nadharia husika zilizotolewa na Albert Einstein.
2. Bw. Demis Hassabis
Mwanzilishi wa kampuni ya DeepMind inayomilikiwa na kampuni ya Google amefuatiliwa baada ya programu ya AlphaGo kushinda mshindi wa dunia wa mchezo wa Go Bw. Lee Sedol kutoka Korea Kusini.
3. Dr. John Zhang
kutoka kituo cha uzazi cha New Hope cha Marekani na kikundi chake wakitumia teknolojia ya kuhamisha kiini cha seli wamemsaidia mama kuzaa mtoto mchanga mwenye jeni kutoka watu watatu. Teknlojia hii inamsaidia mtoto asirithi magonjwa yanayosababishwa na tatizo la Mitochondria zilizopo kwenye seli.
4. Dk. Celina M. Turchi
Dk. Celina M. Turchi na madaktari wengine walifanya utafiti mwingi katika eneo linalosumbuliwa na magongjwa ya Zika nchini Brazil, na kuthibitisha uhusiano kati ya maambukizi ya virusi vya Zika kwa mama katika miezi mitatu ya mwanzo ya kipindi cha ujauzito na kuzaa kwa mtoto mchanga mwenye ugonjwa wa kichwa kidogo.
Wanasayansi wengine walioteuliwa kwenye orodha hii ni pamoja na:-
5. Bw. Terry Hughes mtafiti wa matumbawe ,
6. Bw. Guus Velders mtaalamu wa kemikia ya hewa ,
7. bibi. Alexandra Elbakyan mwanzilishi wa tovuti ya Sci-Hub ,
8. Kevin Esvelt mwanabiolojia ,
9. Guillem Anglada- mwanajimu Escude, na
10, Elena Long. mwanafizikia
Marejeo: coralcoe.org na Tovuti ya China Radio International,