Zikiwa zimesalia siku chache kuukamilisha mwaka 2016 na kuhukaribisha mwaka 2017, TeknoTaarifa inakufahamisha Teknolojia na Vifaa vilivyozinduliwa na Kampuni ya Google Mwaka 2016
1. Google Pixel na Pixel XL
1. Google Pixel na Pixel XL
Hizi ni simu mpya ambazo zitachukua nafasi ya simu
aina ya Nexus 5X na Nexus 6P. Zitakuwa baadhi ya simu za kwanza kabisa
kutumia mfumo wa Android usioambatanishwa na teknolojia zingine, yaani
Android ya kipekee.
Pixel XL imekuja na screen wa inchi 5.5 na
vipimo vya pixeli 1440 x 2560 huku pia ikiwa na uwezo mkubwa zaidi wa
kudumisha betri. na
prosesa za hali ya juu aina ya Snapdragon 821, RAM ya 4GB, skena za
vidole, zinajaa moto haraka pamoja na kuwa na kamera ya 12MP. Bei yake
bado haijajulikana.
Daydream ndio mfumo mpya wa Google wa teknolojia ya VR
(Virtual Reality) unaoupa ule wa Samsung Gear VR ushindani wa kikweli.
VR ya Google imekuja na shimo la kuweka waya ya kusikilizia video
unayotazama kwenye maskio.
Inasemekana kwamba kifaa hiki kitauzwa kwa 'bei ya mkulima' ya Sh7,900 ambayo ni ya chini ikilinganishwa na ile ya Samsung.
3. Google Home
Ni teknolojia itakayokuwezesha kucheza muziki kwa
kutoa maagizo ya sauti, kuuliza maswali ambayo Google Assistant
itayajibu kwa ufasaha kulingana na taarifa zilizoko kwenye Google
Search.
Itakuwezesha kudhibiti aplikesheni na vifaa vingine
vilivyounganishwa na simu yako ukitumia sauti bila kuiguza hata kidogo
simu yako.
Hii ni OS mpya ambayo itaunganisha OS za Android na
Chrome na kuongeza ubora wa faili na udhibiti wa Chrome kutoka kwa
kompyuta hadi kwa simu za Android. Andromeda itatumika kwenye tarakilishi za mezani, vipakatalishi, simu na tableti.
Hii ni ruta ambayo itaweza kusambaza mawimbi
ya intaneti bila waya kwa umbali zaidi kuliko Wi-Fi za awali. Ina uwezo
wa kuunganisha mitandao (networks) mingi kuwa mmoja wenye nguvu zaidi na
inaruhusu kutumiwa na watu wengi zaidi hata mtaa mzima.
Huduma hii itawezesha kutazama video kwa live streaming. za 4K na HDR huku ikiwa na
shimo la Ethernet linalowezesha kuwa bora zaidi huduma za kutazama
video za mbashara. Itakuwa na kasi mara 1.8 kuliko huduma zilizoko za live streaming.
Chromecast Ultra utaipata kwa Sh7,000 pekee.
Chanzo: cnet.com, pcadvisor.co.uk na pcmag.com