Sheria moja imependekezwa katika jimbo la New Jersey nchini Marekani ambayo kama itapita watu watatozwa Faini ya dola 50 au siku 15 jela endapo mtumiaji wa simu au tableti kwa utumaji wa meseji, mziki n.k wakati mtu anatembea.
Maeneo ambayo sheria hiyo itabana ni pamoja na maeneo ya barabara – data za nchini Marekani zinaonesha kuna ongezeko kubwa la ajali zinazosababishwa na watembea kwa miguu wanaokuwa wamejikita sana katika utumiaji wa vifaa kama simu wakati wanatembea.
Kosa hilo lililopendekezwa kwa kutumia jina la ‘distracted walking’ tayari lipo katika sheria zinazosuburia kupitishwa kwenye jimbo jingine pia nchini Marekani – la Hawaii, ambapo wao wameweka faini ya hadi dola 250 kama mtu atapatikana na kosa la kuvuka barabara huku akiwa anatumia simu.
Data kutoka bodi ya usalama nchini Marekani inaonesha kulikuwa na kesi za majeruhi 11,101 kati ya mwaka 2000 hadi 2011 zilizosababishwa na utumiaji simu. Huku majeruhi wengi wakiwa wanawake, huku wengi wao wakiwa na umri wa miaka 40 na chini ya hapo.
Mapendekezo ya sheria kama hii yashashindwa kufanikiwa katika majimbo mengine kama vile Arkansas, Illinois, Nevada na New York.
CHANZO: http://researchnews.osu.edu
MHARIRI: AbdallahMagana.com
Topics: HABARI TECH
Imehaririwa na;- Unknown
Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
Playstore
TeknoTaarifa Video
TAARIFA ZILIZOSOMWA SANA
-
Habari yako msomaji wa TeknoTaarifa tuendelee kuhabarishana na kujuzana kuhusu haya maujanja huku kwenye ulimwengu wa teknolojia leo...
-
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema serikali imeamua kufanya jitihada hizo baada ya kubaini kut...
-
ACCOUNTS ASSISTANT I - 2 POSITIONS Qualifications: Possession of Diploma in Accountancy or equivalent ;At least three ...
-
TRA would like to recruit dynamic experienced and qualified personnel to fill vacant positions in the Research & Policy, Human Re...
-
Ref. Na EA.7/96/01/H/68 7th September, 2015 VACANCIES ANNOUNCEMENT On behalf of Mwalimu Julius K. Nyerere University of Science ...
-
Kwa kawaida wajasiriamali wengi hasa wadogo wadogo huzingatia mipango ya kukuza mitaji, kuimarisha uwezo wa wafanyakazi, kukuza faida, k...
-
Regional Manager. TANROADS - RUVUMA is looking for suitable qualified Tanzanian candidates for 11 posts available at Luhimba and...