Header ads

Header ads
» » » Ifahamu Google Earth programu ya ramani na habari ya kijiografia


Google Earth ni programu ya habari kuhusu dunia isiyokuwa bayana , ramani na habari ya kijiografia ambayo awali iliitwa EarthViewer 3D, na iliundwa na Keyhole, Inc, kampuni iliyonunuliwa na Google mwaka wa 2004. Inatengeza ramani ya dunia kwa kupachika picha zilizopatikana kutoka kwa picha za satelaiti, picha za angani na za pande 3 za GIS. Inaendeshwa kwa leseni tatu tofauti: Google Earth, toleo lisilolipiwa na lililo na uwezo mdogo wa utekelezaji; Google Earth Plus (ilisimamishwa) ambayo ina matumizi zaidi; na Google Earth Pro ($ 495 kwa mwaka), ambayo imelengwa kwa matumizi ya kibiashara.
Explore Redwood Trees in 3D
Huduma hii, ambayo ilizinduliwa kama Google Earth mwaka wa 2005, hivi sasa inapatikana kwa matumizi katika kompyuta za kibinafsi zilizowekwa programu za Windows 2000 au zaidi, Mac OS X 10.3.9 na zaidi, Linux Kernel: 2.4 au toleo la baadaye (lililotolewa tarehe 12 Juni 2006) , na FreeBSD. Google Earth inapatikana pia kama {0 kisakuzi kiunganishi} ambacho kilizinduliwa tarehe 28 Mei 2008 Ilianza pia kupatikana kwenye iPhone OS 27 Oktoba 2008, bila malipo kutoka hifadhi ya programu. Mbali na kuibua programu zilizoiimarishwa na Keyhole, Google pia iliongeza picha kutoka kwa hifadhidata yake ya Dunia, kwa programu yao ya kutengeza ramani. Mfunguo wa Google Earth Juni 2005 kwa umma ulisababisha ongezeko mara dufu la kuangaziwa na vyombo vya habari dunia isiyokuwa bayana kati ya 2005 na 2006, kuhamasisha umma kuhusu teknolojia na programu ya setilaiti ya kukagua dunia.
 Where in the World?
Google Earth huonyesha picha za setilaiti za uangavu tofauti za sura tofauti tofauti ya Dunia, jambo linalowawezesha watumiaji kuona vitu kama miji, nyumba, kutoka juu au kwa upande hanamu, (tazama pia mtazamo wa wa kutoka angani). Kiwango cha uangavu kinachopatikana kinategemea sifa zinazopendeza na umaarufu, lakini sehemu kubwa ya dunia(isipokuwa baadhi ya visiwa)zimefunikwa angalau katika mita 15 za uangavu. Melbourne, Victoria, Australia; Las Vegas, Nevada; na Cambridge, Cambridgeshire ni mifano yenye uangavu wa juu sana, wa sentmita 15 ( nchi6). Google Earth inaruhusu watumiaji kutafuta anwani kwa baadhi ya nchi, kuingia anaratibu, au tu kwa kutumia puku kusakura hadi mahali.
Kwa sehemu kubwa ya uso wa dunia picha za pande 2 tu ndizo zinapatikana, kutoka upigaji picha wa karibu wima. Ukitazama kutoka upembe, kuna mtazamo kwa maana kwamba vitu ambavyo viko mbali kwa mlalo vinaonekana vikiwa vidogo, lakini bila shaka ni kama kutizama picha kubwa, sio kabisa kama mtazamo wa pande 3.
Kwa maeneo mengine ya uso wa dunia picha za pande 3 za Mandhari na majengo zinapatikana. Google Earth inatumia data ya digital elevation model (DEM) zilizokusanywa kwa mtambo wa NASA wa Shuttle Radar Topography Mission (SRTM). Hii ina maana mtu anaweza kutazama Grand Canyon au Mlima Everest katika pande tatu, badala ya pande 2 kama maeneo mengine. Tangu Novemba 2006, mitazamo ya pande 3 ya milima mingi, ikiwemo mlima Everest, imeboreshwa kwa kutumia data za DEM kujaza mapengo katika habari ya SRTM.

Watu wengi hutumia programu kuongeza data zao wenyewe, kwa kuzifanya kupatikana kupitia vyanzo mbalimbali, kama vile Bulletin Board Systems (BBS) au blogu zilizotajwa katika sehemu ya viungo hapo chini. Google Earth inaweza kuonyesha kila aina ya picha zikiwa zimepachikwa juu ya uso wa dunia na pia ni programu ya Web Map Service. Google Earth inasaidia katika kuratibu data ya satelaiti ya kukagua dunia kwa kupitia Keyhole Markup Language (KML).

Google Earth ina uwezo wa kuonyesha picha za pande 3 za majengo na miundo (kama vile madaraja), ambayo inajumuisha michoro iliyowasilishwa na watumiaji kwa kutumia SketchUp, ambayo ni programu ya kutengeza vielelezo katika pande 3. Katika matoleo awali ya Google Earth (kabla ya toleo la 4), majengo ya pande 3 yalikuwa yanapatikana katika miji michache , na yalionekana vibaya, bila umbo. Majengo na miundo mingi Duniani sasa ina miundo naganaga ya pande 3; zikiwemo (lakini siyo tu ) Marekani, Canada, Ireland, India, Japan, Uingereza, Ujerumani, Pakistan na miji ya, Amsterdam na Alexandria. Katika Agosti 2007, Hamburg ukawa mji wa kwanza kuonyeshwa kabisa katika pande 3, pamoja na umbo kama gao. Mji wa Westport wa Ireland uliongezwa kwa Google Earth katika pande 3 mnamo 16 Januari 2008. Kielelezo cha 'Westport3D' kiliundwa na kampuni ya kuchukua picha za pande 3 ya, AM3TD kwa kutumia teknolojia aina ya leza ya kulenga mbali na kuchukua picha za dijitali na ni kielelezo cha kwanza cha mji wa Ireland kuundwa. Kwa vile awali iliundwa ili kusaidia Serikali ya Mtaa katika kuendesha kazi ya kupanga mji inajumuisha mfumo wa kupiga picha za kipekee za kuaminika zenye uangavu wa hali ya juu sana kuwahi kupatikana katika Google Earth. Picha za pande tatu za majengo na miundo zinapatikana kote duniani kupitia hifadhi ya picha za pande 3 za Google na tovuti nyingine.
Add your local knowledge to the Map
Google iliongeza kipengele kinachoruhusu watumizi kutazama mbio za magari katika vizuizi vilivyo yadi 200 katika wakati halisi. Katika toleo la 4.3 lililozinduliwa 15 Aprili 2008, kifaa cha kukuzia picha cha Google Street View kiliunganishwa kikamilifu katika programu na kuiwezesha programu hiyo kutoa mtazamo wa kiwango cha mtaani katika maeneo mengi.
Tarehe 17 Januari 2009, picha zote za Google za sakafu ya bahari zilitengenezwa upya na SIO, NOAA, jeshi la wanamaji la US , NGO, na GEBCO. Picha hizo mpya zimesababisha visiwa vidogo kama vile vya Maldives, kutoweza kuonekana licha ya kuwa fuo zao zimelainishwa kabisa.
Tarehe 21 Oktoba 2009, picha za eneo zima la Poland zilitengenezwa upya (sehemu nyingi zilitatiza kuonekana katika uangavu wa chini, sasa zimeshatengenezwa upya), na - katika maeneo mengine - zimeshushwa (katika uangavu mzuri sana, sasa ni wa kadri).

MAREJEO (Refference) : Google Earth Product Family &
Web User-Google Earth interview.

MHARIRI: AbdallahMagana.com

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post