Napozungumzia ulinzi thabiti katika kompyuta na simu simaanishi
kuweka kampuni ya walinzi au kuajiri watu kwa ajiri ya kulinda kompyuta
yako, hapana!. Hapa nazungumzia ulinzi wa ndani wa kompyuta yenyewe na
taarifa (data) zilizo ndani yake. Kwa jamii yetu ni ngumu sana kuelewa
umuhimu wa Antivirus kwa vifaa vyetu kama
kompyuta na simu,
Suala la kuwa na programu bora kabisa ya
Antivirus ni kukukinga na mashambulizi yote ya vijidudu vinavyoweza
kutumika kudukua data zako au kupunguza ufanisi wa kompyuta yako.
Nimeamua kukuletea orodha ya Antivirus 10 bora zilizopimwa
Kwa ufanisi wake na wataalamu wa mambo ya usalama wa kimtandao kama jarida
maarufu la habari za kiteknolojia la pcmagazine linavyoeleza.
Hivi ni baadhi ya vigezo vilivyotumika kupata orodha hii
- Matokeo ya Maabara za kompyuta zilizopima ufanisi wa kila Antivirus iliyo sokoni kwa sasa
- Idadi ya mashambulizi inayoweza kukamata kwa dakika
- Uwezo wa kukulinda na mashambulizi ya kimtandao moja kwa moja bila usaidizi wa programu nyingine
- Urahisi wa kutumia
- Kiasi cha diski hifadhi na memory inayotumia (hapa katika kuongeza ufanisi wa kompyuta husika)
- Huduma za nyongeza kama kulinda miamala yote ya kifedha mtandaoni (e-money transfer protection)
1. Bitdefender Antivirus Plus 2016 (Bei $39.96 3 Users)
Bitdefender Antivirus Plus 2016 imeongoza orodha hii kwa kupata matokeo mazuri kutoka maabara pamoja na maoni ya watumiaji duniani kote. Uwezo wake wa kupambana na Virusi pamoja na worms wa aina zote kwa haraka na bila kuichosha kompyuta ya mtumiaji kumeifanya Bitdefender kukamata nafasi ya kwanza katika orodha hii.
2. Kaspersky Antivirus 2016 (Bei $39.95)
Nadhani Kaspersky ndio Antivirus inayotumika zaidi ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki, ikiwa imebeba jina la mgunduzi wake Eugen Kaspersky raia wa Urusi imeshika nafasi ya pili katika orodha hii. Kikubwa katika programu hii ni uwezo wake wa kuzuia mashambulizi ya moja kwa moja kutoka ndani ya kompyuta yenyewe, vifaa vinavyochomekwa au kutoka mtandaoni.
3. McAfee Antivirus Plus (Bei $59.99)
McAfee Antivirus ni nzuri zaidi, ila kikubwa kinachoibeba katika orodha hii ni uwezo wake wa kufanya kazi katika matoleo yote ya mifumo endeshi ya Mac, Windows, Linux , iOS pamoja na Android kwa CD ile ile moja uliyonunua na kuinstal katika vifaa vyako vyote hivyo bila wasiwasi.
4. Webroot SecureAnywhere Antivirus (Bei $39.99)
Matokeo kutoka maabara zote maarufu zinazojihusisha na kupima ufamisi wa programu za Ulinzi wa kompyuta zimeibeba Antivirus hii ambayo ni ngeni miongoni mwa watumiaji wengi wa ukanda huu. Inasifika kwa uwezo wake wa kukamata na kuondoa kabisa malware (Malicious Softwares)katika kompyuta.
5. Avast Pro Antivirus 2016 (Bei $34.99)
Bado watumiaji wengi wanaimani na Avast japo imeshindwa kufanya vizuri katika miaka ya karibuni. Miaka mitano iliyopita Avast ilikuwa ikishika namba moja katika antivirus zenye uwezo mkubwa wa kupambana na virusi vya aina zote. Ugumu katika utumiaji kumeifanya Avast izidi kushuka kila mwaka.
6. AVG Antivirus 2016
7. Daily Safety Check Home edition
8. Emisisoft Anti-Malware 10.0
9. ESET NOD32 Antivirus 9
10. F-Secure Antivirus 2016
Matokeo haya ni kama yalivyotelewa na maabara za West Coast Labs, Virus Bulletin, ICSA Labs, Dennis Technology Labs, AV-Test Institute, na AV-Comparatives.
Antivirus kama Avira, Norton pamoja na G-Data yanakosekana kwenye orodha hii sababu hayajapitiwa bado na maabara tajwa hapo juu.
CHANZO: pcmag.com
MHRIRI: AbdallahMagana.com