Teknolojia hii imetokea wapi?
Huko
nchini Japan kuna mahekalu ya kitamaduni ambayo huvunjwa na kujengwa
upya kila baada ya miaka 20. Kitu cha pekee katika ujengaji wa hekalu
hizo no utumiaji wa mbao usiohusisha utumiaji wa ata msumari mmoja
katika ujenzi wake.
Teknolojia hiyo inatumika kwa miaka mingi katika ujengaji wa hekalu maarufu Japan – The Ise Grand Shrine
Ubomoaji na ujengaji wa mahekalu hayo umekuwa ukifanyika kwa takribani miaka 1,300 sasa,
na huwa wanabomoa na kujenga tena ili kuhakikisha majengo hayo
yanaendelea kuwa na nguvu na usalama. Teknolojia ya ujengaji huo
inapitia kwa vizazi hadi vizazi, na sasa Toyota wanatumia teknolojia
hiyo katika utengenezaji wa gari.
Wiki ya Ubunifu mjini Milani, Italia
Takribani mwezi kuanzia sasa kutakuwa na
maonesho ya ubunifu katika jiji la Milani, (Design Week in Milan,
Italy) na ndio Toyota wanategemewa kutambulisha gari hilo rasmi litakalotambulika kama Sersuna.’
Ubunifu wa gari hilo ambao wameuita
Setsuna, unaonesha kitu ambacho wanaweza kukifanya baadae. Wanashiriki
maonesho hayo ili pia kuweza kupata mitazamo kutoka wabunifu wengine.
Aina kadhaa za mbao zimetumika kutengeneza bodi la gari hilo, chasis, viti, uskani (steering wheel) na rim za matairi.
Picha ya designer na the engineer wa gari ilo (Picha: Bertel Schmitt)
Je mbao hizo zimejishakaje kama misumari na ‘screw’ hazijatumika?
Ni uunganishaji wa sehemu zinazokutana
kwa kutumia maumbo ya ‘concave’ na ‘convex’ (umbo la mbonyeo) ndio
vinavyoshikanisha sehemu mbalimbali za gari hilo.
CHANZO: forbes.com
MHARIRI: Abdallahmagana.com