Hapa naongelea zile program zisizotakiwa ambazo zinachukua mamlaka katika vivinjari kama vile Google Chrome na Mozila firefox na kuonyesha matangazo mengi sana kipindi unapotembelea mitandao tofauti tofauti katika kompyuta yako.
Siongelei matangazo yale ya kawaida kama yale unayoyaona Facebook na Google wameyaweka katika mitandao yao.
Matangazo haya mara nyingine huwapeleka watu moja kwa moja katika maduka makubwa ya kimtandao kama vile Target, Walmart na Aliexpress, na mara nyingine matangazo hayo yanaweza kusababisha kuweka kwa programu chafu kwenye kompyuta yako pale unapoyabofya.
Mtu ambaye kashawahi kuona kioo cha kompyuta yake kinaonekana kama hivi ina maanisha ameshakumbwa na tatizo hili ( Picha na technorms.com)
Jizuie Kupata Program Hizo Za Matangazo
Habari nzuri ni kwamba makampuni mengi
ya teknolojia wameweka njia mbalimbali za kuzuia au njia za kiusalama
katika software zao kwa mfano Google wana Safe Browsing ambayo
inawasaidia watu wenye Chrome, Firefox au Safari kutoweza tembelea
mitandao yenye tuhuma mbaya na kushusha ‘software’ mbali mbali bila
kibali
Lakini kuna kitu kingine ambacho watu
wanaweza fanya ili kujikinga wenyewe. Watu wenye kompyuta inawabidi
watumie programu endeshaji (OS) ambazo ni mpya zaidi na kuboresha
vivinjari vyao kwa kushusha matoleo mapya. Hali hii itasaidia kompyuta
yako kwa ujumla kwa kuwa kila toleao jipya lina marekebisho ya kukulinda
zaidi.
- Kuwa na uchaguzi juu ya kitu gani unashusha (unadownload) ni njia nyingine ya kujikinga.
- Kusoma vigezo na masharti ni vigumu ndio! lakini jitahidi kusoma inaweza kukusaidia kujua vitu vingi katika hiyo program au software kabla hata hujaanza kuitumia
- Kama linki au mtandao wowote unaonekana sio ya kawaida basi usishushe kitu chochote kutoka katika mtandao au linki hiyo.
- Kama katika kuweka programu (install) inakuwa inakupa matangazo mengi achana nayo au kuwa mwangalifu, epuka kubofya kwenye matangazo hayo.
Licha ya hayo yote ni vizuri kushusha programu au apps katika mitandao ambayo ni rasmi.
Jinsi Ya Kutoa Programu Hizo Za Matangazo
Chaguo lako la kwanza ni kushusha ‘software’ ambayo itakusaidia kuondoa hayo yote kwa ajili yako. Avast ni ya kuaminika na ya bure. Pia unaweza lipia ‘Software’ katika makampuni ya usalama kama vile Bitdefender, Symantec na Kaspersky.
Watumiaji wa Chrome katika windows wanaweza tumia ile software removal tool ya Google. Apple wameelezea njia juu ya kufuta programu hizo hata Windows nao walitoa maelezo juu ya watu kutoa program hizo wenyewe katika kompyuta zao.
Mara tuu baada ya programu hizo kuondolewa katika kompyuta yako ni vizuri kuanza upya kutumia vivinjari vyako kma ni Chrome, Firefox, Internet Explorer au Safari.
Usijisikie vibaya kwa sababu ‘hakuna njia rahisi’ ya kuepukana na hali hii. Ni kweli inawakumba watu wengi sana na pia inakera. lakini haidhuru kwa watu kuwa makini.