Rafiki Unavuta sigara na
unatamani kuacha kuvuta na umeshindwa au ulikua unavuta sigara na
umefanikiwa kuacha bado kuna tatizo lililobakia nalo ni kuweza kujizuia na
matamanio ya kuvuta tena. Kujikinga na matamanio (arosto) ni vigumu sana lakini
unaweza kujitahidi na kuachana nayo kabisa.
App ya Kwit inafanya kazi kama vile
Gemu katika kifaa chako katika kuboresha mazingira ya kukusaidia kujidhibiti na
hamu ya kuvuta na kuacha kuvuta kabisa.
Utaweza kupata pointi na hatimaye
kupiga hatua kadha wa kadha na hii itatokana na siku ambazo hujavuta sigara.
unaanza kutumia App hii kama mtawaliwa na sigara na unamaliza kama mwachaji
kabisa wa sigara Muonekano Wa App Ya Kwit Ukiwa unaendelea utaona afya yako
inabadilika na unaanza pata pointi nyingi, mfano katika daraja (level) la 5
kaboni monoksidi inatolewa mwilini *ndani ya gemu* Kama bado ukiwa unataka
faraja na vitu mbalimbali vya kutia moyo App hii ya Kwit ina kadi 200 zilizojaa
maneno ya motisha tupu, ambayo yatakusaidia kuhakikisha unapata motisha wa
kutosha.
Na kwa kupata faraja zaidi hata kwa
wanaokuzunguka unaweza sambaza maendeleo yako kutoka Kwit kwenda katika
mitandao ya kijamii. Hapa unaweza pata pongeza na hata kukosolewa na watu na
kupewa moyo pia, lakini hii yote itategemea unaitumia App ya Kwit namna gani.
Kama maendeleo ni mazuri ni lazima utapata pongezi Lakini pia kitu kikubwa
unachopata kutoka App ya kwit ni taarifa muhimu zinazokuhusu wewe.
Katika dashibodi ya Kwit utaona ni
sigara ngapi hujavuta, kiasi gani cha pesa umeweza okoa na pia siku ngapi
umeweza ongeza katika maisha yako…. burudani tosha.
App ya kwit inapatikana katika
AppStore kwa watumiaji wa iOs , watumiaji wa masoko mengine wakae mkao wa kula
kwani itaingia mpaka katika masoko yao. Kuvuta sigara licha ya kuwa kunapigwa
marufuku bado kuna watumiaji wengi, njia nyingi za kuzuia hili tatizo zipo. Na
hapa ndipo teknolojia nayo ilipochukua nafasi yake katika hili. Kuna App
mbalimbali zinazopinga matumizi ya sigara Kwit ikiwa moja wapo.
Nimekuwekea
Video ya Maelezo Kuhusu App ya Kwit