Header ads

Header ads
» » Wanasayansi wa Australia waunda kifaa cha jicho kinachoweza walemavu wa macho kuona

Habari njema kwa walemavu wa macho!

Wanasayansi wa chuo kikuu cha Monash kilichoko mjini Clayton nchini Australia, wameunda kifaa cha jicho kinachoweza kunasa picha na kuisafirisha hadi ubongoni.
Kifaa cha jicho kilichounganishwa kwenye miwani ya kamera, kitawawezesha walemavu wa macho kuona mazingira ya dunia japo kwa kiasi kidogo.
Kwa kuzingatia muundo wa kifaa hicho, vibati 11 vidogo vilivyobobea vinasio 43 vya elektrodi kwa kila kimoja vinasemekana kuwa na uwezo wa kuunganisha mawasiliano ya picha hadi kufikia ubongoni.
Vibati hivyo vinaweza kutuma ishara ya picha zenye ubora wa pikseli 500 ubongoni.
Muundo huu na uwezo wa kunasa picha kwa ubora wa kiwango hicho ukilinganishwa na ubora wa picha wa pikseli milioni 1.5 unaotokana na kiini cha jicho, unaweza kuashiria mfano wa picha za filamu za vibonzo.
Wakati huo huo, watu wenye ulemavu wa macho wataweza kutambua vitu mbalimbali kwenye mazingira kwa urahisi kwa kutumia picha hizo chache zinazonaswa na kifaa cha jicho. 
Wanasayansi wametoa maelezo na kusema kwamba kifaa hicho cha jicho huenda kikatatua tatizo la ulemavu wa macho ikiwa maboresho yatatimia kwa mafanikio.
Kifaa hicho cha jicho kinatarajiwa kufanyiwa majaribio kwa walemavu wa macho watakaojitolea.


References and useful resources:  
CNN News

>>>Tafadhali Click link zifuhatazo kuhungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM  

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post