Kuna Smartphone yenye uwezo wa kukaa na chaji kwa zaidi ya siku 10?. Haraka haraka jambo hili linaonekana bado ni ndoto ila tayari kuna kampuni ambayo imedai imefanikisha jambo hili na simu zake zitaanza kupatikana mapema mwezi wa kwanza, 2016. Smartphone hiyo inakuja na betri lenye kiwango kikubwa cha uhifadhi chaji wa mAh 10,000 italetwa na kampuni iitwayo Oukitel.
Wenyewe wanasema kwa matumizi ya ‘kawaida’
wanategemea simu hiyo iweze kukaa na chaji kwa zaidi ya siku 10,
wanasema kutegemea na utumiaji inaweza fikisha hadi siku 15.Kampuni hiyo
tayari miezi kadhaa nyuma ilishawahi kutoa simu janja yenye kiwango
kikubwa cha uhifadhi chaji wa mAh 6000. Simu hii ya kiwango cha chaji
cha mAh 10,000 itachukua jina la Oukitel K10000 na inakuja ikitumia
toleo la Android 5,1 Lollipop.

Sifa zinginezo za Oukitel K10000
• Kioo (display) ya Inchi 5.5 HD (720X1280)
• Prosesa – 1GHz quad-core MediaTek MT6735
• RAM GB 2
• Diski Uhifadhi (Storage) – GB 16 na uwezo wa kutumia kadi ya microSD
• Kamera ya mbele ya MegaPixel 8 na ya
selfi MegaPixel 2 Kamera ya mbele inakuja na teknolojia za HDR, kutambua
sura (face detection), uwezo wa kupiga picha za panorama n.k
Kimawasiliano inakuja na teknolojia za
GPRS/EDGE na 3G, pia Bluetooth na WiFi. Kwa sasa simu hiyo ishaanza
kuuzwa kupitia mtandao wa GearBest kwa takribani dola 240 za Marekani,
wanaolipia kwa sasa wataanza kuipata simu hiyo mwezi wa kwanza ambapo
ndio pia itaanza kupatikana katika nchi zingine.
>>>Tafadhali Click link zifutazo kuhungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM
>>>Tafadhali Click link zifutazo kuhungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM