
Zaidi ya miaka 42 iliyopita simu ya kwanza ilipigwa kutumia simu ya mkononi, simu hiyo ya kwanza ya mkononi ilitengenezwa na kampuni ya Motorola. Ilikuwa mwezi wa 4 tarehe 3 mwaka 1973 walijaribu kupiga simu kwa kutumia simu hiyo ya kwanza ya mkononi iliyokuwa inafahamika kwa jina la Motorola DynaTAC. Mfanyakazi wa Motorola aitwaye Marty Cooper alitumia simu ya mkononi kupiga simu kwenda ofisi yao (kwenye simu ya mezani), ilipoita na kupokelewa alisema, “Napiga simu kutaka kufahamu kama nasikika vizuri upande huo.”
Bwana Martin Cooper akishikilia Motorola DynaTAC kushoto
kwake na simu yake nyingine aliyokuwa anatumia, picha hii ni ya mwaka 2009.
Simu hii ilikuja kuingia sokoni mwaka 1983 baada ya muda
kidogo ikitumia jina la Motorola DynaTAC 8000x na hii ndiyo simu ya kwanza ya
mkononi kuingia sokoni na watu kuweza kununua. Na ilikuwa inauzika kwa bei ya
juu sana,
dola 3995 za kimarekani za wakati huo, ambayo ni si chini ya
Tsh 8,000,000 za kitanzania. Mafanikio ya simu hii ilifanya yatoke matoleo mengine
kadhaa ya maboresho zaidi,
Fahamu sifa za Motorola DynaTAC 8000x Ilikuwa inatumia
teknolojia ya analogia hivyo haikuwa na uwezo wa kuwekwa laini, teknolojia
ilikuwa haijafikia huku. Ilikuwa na uzito wa kilogramu 1.1 ukilinganisha siku
hizi simu nyingi zinakuwaga na uzito wa gramu 100 hadi 150 (Kumbuka kilogramu 1
= gramu 1000) Ilikuwa na urefu wa sentimita 33 kwa 8.89 na kawembamba ka
sentimita 4.4. Kioo (display) chake kilikuwa kiduchu, cha kuandika mstari mmoja
tuu. Iliitaji kuchajiwa kwa muda wa masaa 10 kutoka kutokuwa na chaji kabisa
hadi kujaa kabisa Na ata baada ya kuchaji kwa muda wa masaa 10 muda wa maongezi
wa takribani dakika 30 tuu ungemaliza chaji hiyo. Mlinganisho rahisi wa ukubwa
wa simu hii na zingine za kisasa.
References and useful resources:
- 1980s Motorola DynaTAC Promotional Video
- Motorola Executive Helped Spur Cellular Revolution
- >>>Tafadhali Click link zifuhatazo kuhungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM