Taarifa
hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dk. Stephen Kebwe wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti
Maalum, Diana Chilolo (CCM).
Katika
swali lake, Chilolo aliitaka Serikali kupelekea madaktari katika
hospitali ya Ikungi kwa kuwa licha ya kupandishwa hadhi kuwa hospitali
ya rufaa lakini haina wataalamu wa kutosha.
Dk.
Kebwe alisema katika mpango wa Serikali wa kuimarisha hospitali za
rufaa za wilaya, mikoa na kanda kwa sasa inao wataalamu zaidi ya 400
walio vyuoni na kwamba kwa kadri watakavyokuwa wanahitimu watapelekwa
katika hospitali hizo.
Awali
akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Pudenciana
Kikwembe (CCM), Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Utumishi, Celina Kombani
alisema Wilaya ya Mlele ilipewa maelekezo ya jinsi ya kufanya ili kituo
cha afya Iyonga kipandishwe hadhi kuwa hospitali ya wilaya.
“Melekezo
hayo ni pamoja na kuwa na jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhi maiti,
chomeo taka, jengo la maabara, chumba cha mionzi, kuweka mfumo wa maji
safi na maji taka na kufunga mfumo wa umeme kwenye majengo yote ya kituo
cha afya,” alisema.
Kombani
alisema Halmashauri ya Wilaya ya Mlele imeanza utekelezaji kwa kuingia
mkataba na SUMA JKT wa Sh.bilioni 1.6 kuondoa upungufu huo.
Alisema inatarajiwa ifikapo Septemba, 2015 majengo hayo yatakuwa yamekamilika.
Katika swali lake, Dk.Kikwembe alitaka kujua lini kituo cha afya Iyonga kitapandisha hadhi na kuwa Hospitali ya Wilaya ya Mlele.