Wizara ya mambo ya ndani nchini Kenya ikiongozwa na Salim Mahmoud ilifahamisha kuwa kundi la wahandisi linafanya utafiti kuhusu hali ya ardhi ya eneo hilo ili kufahamu kiwango cha vifaa vya ujenzi vitakavyo hitajika.
Baada ya utafiti huo, shughuli za ujenzi zitaanzishwa mara moja.
Ukingo huo unatarajiwa kujengwa bain aya Lamu na Wajir.
Shuhuli za ujenzi zitaanza ifikapo mwezi Julai.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani, Mwenda Njoka alifahamisha kuwa ukingo huo hautokuwa ukuta wa matofali bali nyaya na sinyenge ambazo zinakuwa na umeme.
Mradi wa kujenga ukingo huo umeharakishwa kutokana na kuuawa kwa wanamgambo 11 wa el shabaab Lamu wakitokea Somalia.