Header ads

Header ads
» » Brazil yafungishwa Vilago Michuano ya Copa America

 Brazil yatupwa nje ya Copa America

Ndoto za wana Samba wa Amerika ya Kusini za kuchukua kombe la Copa America ziliyeyuka hapo jana baada ya Paraguay kuwaengua katika mashindano hayo.

Selecao walianza vizuri mchezo huo na kujitahidi kupeleka mashambulio makali katika lango la Paraguaay.
Mkongwe wa timu hiyo, Robinho alifanikiwa kuipatia Brazil bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza cha mchezo.
Lakini goli hilo lilikuja kusawazishwa mnamo dakika ya 67 ya mchezo na kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa.
Brazil waliondoshwa katika matuta wakati Paraguay iliposhinda penati 4 huku Brazil ikipata penati 3 pekee.
Makali ya kinda wa Brazil aliyesajiliwa na Liverpool, Firmino yalishindwa kuonekana katika dakika zote alizocheza.
Kocha wa Brazil, Dunga ameisifu timu yake hiyo kwa kiwango kizuri lakini alilalamikia hali mbaya ya afya ya wachezaji wake ndiyo iliyopelekea kutolewa katika mashindano hayo.
Paraguay sasa itachuana na Argentina katika nusu fainali za mashindano hayo huku wenyeji Chile wakiivaa Peru hapo Jumatatu.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post