Wana mashabiki wengi, miongoni mwao tayari ni mamilionea (wa shilingi),
wapo wenye mijengo, magari ya kifahari, miradi ya biashara, makampuni,
endorsements na vitu vingine. Hawa ndio wasanii 12 wa Tanzania wenye
nguvu zaidi mwaka 2014.
Diamond Platnumz
Diamond Platnumz ndiye msanii anayeandikwa zaidi kwenye vyombo vya
habari Afrika Mashariki kwa sasa. Hadi sasa Diamond amefikia hatua
ambayo haijawahi kufikiwa na msanii yeyote wa Tanzania. Ndiye msanii
mwenye show nyingi zaidi kwa sasa.
Kimataifa 2014 umekuwa wa mafanikio zaidi kwake kuanzia kutajwa kuwania
vipengele viwili kwenye tuzo za MTV MAMA, BET Awards, kushiriki kwenye
wimbo uliokutanisha mastaa takriban 20 wa kampeni ya ‘Do Agric’ ‘Cocoa
na Chocolate, pamoja na wimbo ‘Africa Rising’ uliomkutanisha na wasanii
kama Mi Casa Music, Davido, Sarkodie na Tiwa Savage.
Pia pamoja na kufanya wimbo na Davido, Diamond ameshafanya collabo na
wasanii wengine wa Nigeria wakiwemo Iyanya, Waje na Dr Sid pia hivi
karibuni ameshirikishwa na kundi la Afrika Kusini, Mafikizolo.
Pamoja na kukosa tuzo za kimataifa alizotajwa kuwania, staa huyo mwaka
huu alivunja rekodi kwa kuchukua tuzo zote saba alizotajwa kwenye KTMA
na pia kushinda tuzo za watu zilizotolewa June 27.
Akiwa na video mbili mpya kibindoni, moja ya wimbo aliofanya na Iyanya
na ile ya wimbo wake ‘Mdogo Mdogo’, Diamond ana uhakika wa kuendelea
kuutawala mwaka 2014.
Lady Jaydee
Judith Mbibo aka Lady Jaydee ndiye msanii wa kwanza wa Tanzania
kufikisha likes 300,000 kwenye mtandao wa Facebook huku sasa idadi ikiwa
ni zaidi ya 329,000. Tangia June mwaka jana alipofanya show yake ya
miaka 13 ya muziki wake na kuijaza Nyumba Lounge watu wasipate pa
kukanyaga, Lady Jaydee haoneshi dalili za kusimama. Baada tu ya kutoka
kwenye Coke Studio Africa, Jaydee alishiriki kwenye wimbo maalum
kwaajili ya kombe la dunia wa Coca Cola, ‘The World is Ours’. Pamoja na
show zisizo katika, biashara yake kuu ya mgahawa imeendelea kufanikiwa.
Kwa mujibu wa meneja wake, Gadner G Habash ambaye pia ni mumewe pamoja
na kuwa na biashara yake ya Nyumbani Lounge, Lady Jaydee anatarajia
kuongeza zaidi miradi mingine. “Huyu bado ni mjasiriamali mchanga
anayejifunza zaidi na angependa kufanya biashara nyingi lakini muda ni
mdogo. Isipokuwa kwa mwaka huu alitarajia kufanya kitu kingine kuongeza
kama biashara. Hajawa tayari kusema ni kitu gani lakini mwenyezi Mungu
akijaalia heri na afya mwaka huu kuna biashara nyingine Jaydee
ataitambulisha, ukiacha Nyumbani Lounge na muziki,” Gadner aliiambia
Bongo5 kwenye mahojiano maalum.
Mwaka huu Jide alipata pia endorsement kutoka kwenye kampuni ya vipodozi
ya Sweden Oriflame Cosmetics na kuungana na wanawake wengine watatu
maarufu wa Afrika Mashariki kuwa mabalozi wa bidhaa zao katika nchi zao.
“Lady Jaydee, Juliana and Jamila have been named because their style
and approach to beauty is the ideal representation for the Oriflame
brand. They are strong and talented women who many people across East
Africa readily identify with,”alisema mkurugenzi mtendaji wa kampuni
hiyo Afrika Mashariki Mr. Klas Kronaas wakati akiwatangaza.
June 28, Lady Jaydee alikuwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza kwenye tukio
la Masaku Rugby 7s After Party lililofanyika huko Machakos Kenya.
Takriban watu 40,000 walihudhuria kwenye show hiyo iliyodhaminiwa na
Tusker Lager. Wasanii wengine walitumbuiza ni pamoja na Jua Cali, Radio n
Weasel, Wyre, Kidum, Keni wa Maria.
Kingine ni kubwa ni kuwa Lady Jaydee ataungana na Ali Kiba kutoka Tanzania kupanda jukwaa moja na Nicki Minaj, J Cole na wasanii wengine wa Marekani na Afrika kwenye tamasha la TribeOne Dinokeng litakalofanyika September mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Kingine ni kubwa ni kuwa Lady Jaydee ataungana na Ali Kiba kutoka Tanzania kupanda jukwaa moja na Nicki Minaj, J Cole na wasanii wengine wa Marekani na Afrika kwenye tamasha la TribeOne Dinokeng litakalofanyika September mwaka huu nchini Afrika Kusini.
AY
Kimuziki mwaka 2014, AY ameendelea kufanya movements nyingi ikiwa ni
pamoja na kuachia wimbo wake ‘Asante’. Akiwa amebobea zaidi katika
shughuli za ujasiriamali, mwaka 2014 umekuwa mzuri kibiashara kwake
kutokana na kupata endorsement kuwa ikiwemo ile ya kampuni ya Samsung.
Pia aliungana na Diamond kwenye mradi wa ‘Do Agric’ wa One Campaign.
Hivi karibuni pia, AY ambaye jina lake halisi ni Ambwene Yessaya pamoja
na aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Faraja Kotta Nyalandu, waliteuliwa kuwa
mabalozi wa UNICEF Tanzania katika mradi wa kupiga vita ukatili kwa
watoto.
Akiwa mmoja wa waanzilishi wa kipindi cha TV kilichoshinda tuzo za watu, Mkasi, AY ana mpango wa kukivukisha boda.
Kwa mujibu wa mtandao wa Nairobi Wire, mwaka huu AY alienda Kenya na crew ya Mkasi inayomjumuisha mtangazaji Salama Jabir na Josh Murunga, kwa ajili ya kuangalia fursa zinazoweza kupatikana nchini humo kwa lengo la kutaka kupanua wigo wa kipindi hicho. “Tuko hapa kwanza kuangalia uwezekano wa kupanua biashara ya kipindi chetu” alisema AY.
Kwa mujibu wa mtandao wa Nairobi Wire, mwaka huu AY alienda Kenya na crew ya Mkasi inayomjumuisha mtangazaji Salama Jabir na Josh Murunga, kwa ajili ya kuangalia fursa zinazoweza kupatikana nchini humo kwa lengo la kutaka kupanua wigo wa kipindi hicho. “Tuko hapa kwanza kuangalia uwezekano wa kupanua biashara ya kipindi chetu” alisema AY.
Hata hivyo, kuna mambo mengi makubwa yanayoendelea katika himaya ya rapper huyo ambayo bado hajayaweka hadharani.
Nay wa Mitego
Nay wa Mitego ni rapper anayeendelea kuwashangaza wengi kwa mafanikio
yake makubwa kimuziki na maisha yake binafsi. Rapper huyo ameendelea
kuwa miongoni mwa rappers wa Tanzania wenye mashabiki wengi nchini huku
nyimbo zake zikiwa na ushawishi mkubwa. Hivi karibuni, aliungana na
Vanessa Mdee na Barnaba kama mabalozi wa kampeni ya Switch On ya Airtel.
Aliwashangaza watu wengi zaidi baada ya kuonesha nyumba yake ya kifahari
aliyoijenga kwa takriban shilingi milioni 150 huku pia akimiliki magari
ya bei.
“Gari yangu mpya Nissan Murano nimenunua milioni 36, ni gari ambayo
naipenda sana ,dream car yangu kwenye maisha yangu ni Murano , ninaweza
nikabadilisha nikawa na gari nyingine, pia mimi napenda nyumba nzuri
,napenda kuishi kwenye nyumba nzuri, nina nyumba tatu, hii hapa ambayo
nahamia kesho ina thamani ya shilingi milioni 170 kila kitu, lakini
inaweza ikawa zaidi ya milioni 170 kwasababu kuna vitu vingine huwa
sivipigii hesabu,” Nay aliiambia Bongo5.
Vanessa Mdee
Vanessa Mdee aliwahi kuiambia Bongo5 kuwa mafanikio aliyoyapata sasa
hakuwahi kuyafikiria. “Nilikuwa natarajiwa makubwa lakini haya ni
makubwa haswaa. Ukiwa unafanya kazi ya muziki you hope for things to
work out, you hope for things to be beneficial. Kwahiyo naona kama
taratibu muziki wa Tanzania umebadilika na wasanii wameanza kupewa
kipaumbele so I am just happy to do what I love to do,” alisema.
Mafanikio hayo ni pamoja na kushinda tuzo ya KTMA, kushiriki kwenye
tour, kufanya matangazo ya biashara, kuchaguliwa kushiriki msimu wa pili
wa Coke Studio Africa, kuhusishwa kwenye kipindi cha Introducing cha
Channel O na mengine. Pamoja na kuwepo watu waliokuwa na mashaka na
kipaji chake, Vee Money ameendelea kuwashangaza wengi na kujikusanyia
mashabiki wa kila aina.
“Mpaka leo wapo wenye mashaka na mimi. Hainikatishi tamaa bali inanipa
changamoto kuendelea kuwaprove wrong na kuendelea kufanya kitu kizuri
mpaka wale waliokuwa na mashaka na mimi wakubali waseme ‘yeah she is the
one’. So I don’t mind a few doubters,” anasema.
Ommy Dimpoz
Mwaka huu, Ommy Dimpoz ni miongoni mwa wasanii waliofanya show nyingi za
nje kwa ziara ya Ulaya, Marekani na Asia. Pia amekuwa amekifanya show
nyingi za nyumbani zinazomuingizia fedha nyingi. Diamond, amewahi
kumtaja Ommy kama msanii anayefuata nyayo za mafanikio yake. Hili
limedhihirika baada ya kuachia video ya wimbo wake ‘Ndagushima’
iliyoongozwa na Moe Musa.
Ommy Dimpoz aliiambia Bongo5 kuwa amepata jibu la kwanini kuwekeza na
kufanya video nzuri kuna faida kubwa. Alisema hakutegemea kuwa kuna siku
video yake itakuwa ikichezwa kama kawaida kwenye vituo vikubwa vya TV
barani Afrika.”Kupigwa video kwenye channel kubwa sio tatizo, video
nyingi sasa hivi zinaenda lakini unawashawishi vipi wakupe pia rotation?
Ni Uzuri wa video, pengine wanaangalia director amefanya nani,”
alisema.
Mwaka 2014, Ommy ameandaa show nyingi zake mwenyewe bila kutegemea promoter na hivyo kuingiza fedha nyingi zaidi na pia kumsaidia kuwa miongoni mwa wasanii wanaochaji fedha nyingi kutumbuiza.
Mwana FA
Hamis Mwinjuma aka Mwana FA ni msanii anayeongoza kwa kuyafanya mashairi
ya nyimbo zake kugeuka sentensi kwenye midomo ya watu wengi. Mwaka huu
wimbo wake ‘Mfalme’ umeongelewa zaidi mitandaoni na kuupa heshima ya hit
isiyohitaji maswali.
FA ameendelea kuwa mchawi wa steji na mara nyingi yeye na AY wameendelea
kuwa miongoni mwa rappers wakali jukwaani. Shughuli nyingi binafsi
anazofanya Mwana FA zimeendelea chini ya kapeti lakini kuna mambo
makubwa anayoyafanya.
Profesa J
Mwaka 2014, Mchawi wa Rhymes, Profesa Jay amerejea tena kwenye chart kwa
ngoma yake ‘Kipi Sijaskia’ aliyomshirikisha, Diamond. Profesa
ameendelea kujiimarisha kwenye miradi mbalimbali ya biashara ikiwa ni
pamoja na kufungua studio yake ‘Mwanalizombe Recs’.
Pamoja na muziki, mwaka huu Profesa aliteuliwa kuwa mmoja wa mabalozi wa
taasisi ya kilimo isiyo ya kiserikali (Ansaf) ambao hivi karibuni akiwa
na AY walimkabidhi Rais Kikwete taarifa ya maoni kutoka kwa wakulima wa
Tanzania, katika mkutano wa maswala ya kilimo uliyofanyika ndani ya
hotel ya Double Tree.
Joh Makini & Nick wa Pili
Kwa mwaka 2014, Joh na mdogo wake Nick wamekuwa wakifanya mambo mengi ya
muziki pamoja. Mwaka huu Weusi wamekuwa rappers wa Tanzania wenye video
kali zaidi kuliko wote na zilizofika mbali. Walianza na ile
iliyoongozwa na mshindi wa tuzo za watu, Nisher ya wimbo wao ‘Nje ya
Box’ iliyoandika historia kwa kuwa video yao ya kwanza kuchezwa Channel
O. Hawakusubiri kwa muda mrefu kwa kuachia video nyingine waliyoshoot
Kenya ya ngoma yao ‘Gere’.
Pamoja na ngoma za Weusi, ndugu hawa wameendelea kushambulia kwa ngoma
zao binafsi ambapo Nick aliachia wimbo ‘Staki Kazi’ uliopata shavu
bungeni. Naye Joh Makini hivi karibuni aliachia single yake ‘Najiona
Mimi’ aka I See Me’ iliyoendelea kumthibitisha kuwa mchawi wa hip hop.
Weusi wameendelea kujimaarisha katika biashara zao kwa kuingiza sokoni
bidhaa mbalimbali zikiwemo masweta, kofia, miwani na bidhaa zingine.
Fid Q
Fareed Kubanda aka Fid Q ameendelea kuwa rapper mwenye ushawishi mkubwa
si tu kwa mashabiki wa hip hop, bali pia rappers wenzie. Uwezo wake wa
kufikiri, maarifa anayoyapata kutokana na desturi yake ya usomaji wa
vitabu, vimemfanya aendelee kuwa rapper mwenye mashairi makali zaidi
Tanzania.
Pamoja na muziki, Fid ameendelea kujihusisha na shughuli za kijamii
ikiwa pamoja na kusimamia vijana wa Hip Hop Darasa na pia kujihusisha na
utengenezaji wa filamu za makala kuhusu masuala ya kijamii. Moja ya
filamu aliyoshiriki kwa kusimulia ilioneshwa kwenye tamasha la ZIFF 2014
lililomalizika hivi karibuni.
Feza Kessy
Feza Kessy ana bahati ya kuwa msanii wa Tanzania mwenye mashabiki
waaminifu nje ya nchi anayotokea. Uhusiano wake na mshiriki wa Big
Brother Africa 2013, Oneal wa Botswana, umemfanya atengeneze kundi la
mashabiki lijiitalo ‘Ninjas’ ambalo lipo nyuma yake katika shida na
raha. Akiwa masomoni nchini Afrika Kusini, Feza ameendelea kufuata ndoto
yake ya kuwa mwanamuziki mkubwa Afrika.
“Kunakuwa kuna shule, halafu kunakuwa na appearance job nafanya, just to
appear as Feza Kessy , kuchukua picha na mashabiki na vitu kama hivyo.
Pia sometimes nakuwa nafanya shows lakini sanasana inakuwa ni Botswana,”
aliiambia Bongo5. Hivi karibuni, alishoot video ya wimbo wake mpya ‘My
Papa’ na inatarajiwa kutoka hivi karibuni