Header ads

Header ads
» » Kituo cha utafiti wa kilimo Makutupora Mkoani Dodoma.chapiga hatua kwa Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO)


KAMATI ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC) imeridhishwa na  matumizi ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) yenye lengo la kuwakwamua wakulima nchini.
Wajumbe wa kamati hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari wakati walipotembelea shamba la majaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma, walisema hatua iliyofikiwa na watafiti hao ni kubwa hivyo haipaswi kuachwa ikapotea bure. 

Elisa Moses kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe ambaye ni mjumbe wa NBC alisema teknolojia hii ya bioteknolojia ni nzuri na inaonesha uhalisia halisi na inaweza kusaidia changamoto za ukosefu wa chakula iliyopo nchi.

"Binafsi nimefurahi kujionea hali halisi ya teknolojia hii hasa ninapoyaona mahindi haya ya GMO yalivyomakubwa kwani ni muhimu sana katika kukabiliana na ukame uliopo sehemu kubwa nchini" alisema Moses.

Meneja wa shamba hilo, Bakar Mohamed akielezea kuhusu 
shamba hilo.
Mjumbe mwingine wa kamati hiyo kutoka Chemba ya Wanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo, Magdalene Mkocha alisema wamefurahi kuona jambo walilolipitisha linafanyiwa kazi vizuri na linaleta matumaini makubwa kutokana na matokeo ya jaribio hilo.

Alisema wadau wa sekta binafsi wanasubiri kwa hamu kuhusu matokeo hayo baada ya kuthibitishwa na takwimu za kisayansi kwani kwa kuangalia kwa macho mahindi yanaonekana ni bora zaidi.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Kanda ya Kati Dodoma, Sebastian Kandira alisema hapo awali tafiti hizo zilikuwa hazifikishwi kwa wakulima ndio maana zilikuwa hazieleweki vizuri lakini hivi sasa wameanza kuzielewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso alisema wakati wanaanza majaribio hayo kulikuwa na changamoto nyingi kutokana na wadau kutokuwa na uelewa hasa kwa mahindi yaliyobadilishwa vinasaba kikubwa ni mshukuru Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba  kwa kufika katika shamba hili la majaribio ambalo tulipanda mahindi Oktoba 5, mwaka jana na kutupa faraja kuwa kuna kila sababu ya kuharakisha matumizi ya teknolojia hiyo ili iweze kutumika kama zinazofanya nchi zingine zinazofanya tafiti za namna hiyo. 

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post