Header ads

Header ads
» » KWIT program pekee itakayokuwezesha kuacha kuvuta sigara.

 




Rafiki Unavuta sigara na unatamani kuacha kuvuta na umeshindwa au ulikua unavuta sigara na umefanikiwa kuacha bado kuna tatizo lililobakia nalo ni kuweza kujizuia na matamanio ya kuvuta tena. Kujikinga na matamanio (arosto) ni vigumu sana lakini unaweza kujitahidi na kuachana nayo kabisa. 


App ya Kwit inafanya kazi kama vile Gemu katika kifaa chako katika kuboresha mazingira ya kukusaidia kujidhibiti na hamu ya kuvuta na kuacha kuvuta kabisa.


Utaweza kupata pointi na hatimaye kupiga hatua kadha wa kadha na hii itatokana na siku ambazo hujavuta sigara. unaanza kutumia App hii kama mtawaliwa na sigara na unamaliza kama mwachaji kabisa wa sigara Muonekano Wa App Ya Kwit Ukiwa unaendelea utaona afya yako inabadilika na unaanza pata pointi nyingi, mfano katika daraja (level) la 5 kaboni monoksidi inatolewa mwilini *ndani ya gemu* Kama bado ukiwa unataka faraja na vitu mbalimbali vya kutia moyo App hii ya Kwit ina kadi 200 zilizojaa maneno ya motisha tupu, ambayo yatakusaidia kuhakikisha unapata motisha wa kutosha. 


Na kwa kupata faraja zaidi hata kwa wanaokuzunguka unaweza sambaza maendeleo yako kutoka Kwit kwenda katika mitandao ya kijamii. Hapa unaweza pata pongeza na hata kukosolewa na watu na kupewa moyo pia, lakini hii yote itategemea unaitumia App ya Kwit namna gani. Kama maendeleo ni mazuri ni lazima utapata pongezi Lakini pia kitu kikubwa unachopata kutoka App ya kwit ni taarifa muhimu zinazokuhusu wewe.


Katika dashibodi ya Kwit utaona ni sigara ngapi hujavuta, kiasi gani cha pesa umeweza okoa na pia siku ngapi umeweza ongeza katika maisha yako…. burudani tosha.


App ya kwit inapatikana katika AppStore kwa watumiaji wa iOs , watumiaji wa masoko mengine wakae mkao wa kula kwani itaingia mpaka katika masoko yao. Kuvuta sigara licha ya kuwa kunapigwa marufuku bado kuna watumiaji wengi, njia nyingi za kuzuia hili tatizo zipo. Na hapa ndipo teknolojia nayo ilipochukua nafasi yake katika hili. Kuna App mbalimbali zinazopinga matumizi ya sigara Kwit ikiwa moja wapo.

Nimekuwekea Video ya Maelezo Kuhusu App ya Kwit




References and useful resources:  
technewstoday na kwit.fr/
>>>Tafadhali Click link zifuhatazo kuhungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM  

Share to:


Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post