Header ads

Header ads
» » China yahimiza matumizi ya magari yatumiayo umeme, Kuyalinda Mazingira



Mwezi Disemba mwaka jana, Beijing ilitoa tahadhari ya juu mara mbili kutokana na kiwango cha juu cha hewa chafu, na kuyazuia magari kutembea kwa mujibu wa namba witiri au shufwa kwenye vibao vya usajili isipokuwa magari yanayoendeshwa kwa umeme. Agizo la "kuzuia magari yanayoendeshwa kwa mafuta na kutozuia yale ya umeme" limewafanya watu kuanza kufuatilia zaidi "magari yanayotumia nishati mpya", ambayo biashara yake inazidi kuwa nzuri nchini China. Imekadiriwa kuwa mauzo ya magari yanayotumia nishati mpya yamefikia laki 2.2 hadi 2.5 mwaka jana, na kuifanya China kuwa soko kubwa zaidi la magari ya aina hiyo duniani.
Bw. Wang anayeishi katika wilaya ya Haidian mjini Beijing ni mmoja wa wamiliki wa magari hayo ya umeme. Kabla ya kununua gari la nishati mpya mwezi Novemba mwaka jana, yeye alikuwa anamiliki gari moja linalotumia mafuta. Anasema, 

"Gari hili ambalo nimeliendesha kwa zaidi ya mwezi mmoja ni zuri na linaweza kukidhi mahitaji yangu mjini. Mimi ni mwepesi kwa jambo geni, na katika siku ambazo hewa ni chafu sana, nusu ya magari yanayotumia mafuta hayaruhusiwi kutembea, lakini magari ya nishati mpya hayazuiliwi."
Mmiliki huyo wa gari amesema gharama ya kuendesha magari ya nishati mpya kwa umbali wa kilomita moja ni robo ya ile ya magari yanayotumia mafuta.
"Uzuri wa magari ya nishati mpya ni gharama ndogo. Kwangu mimi, kuendesha gari la mafuta kwa kilomita moja kunagharimu Yuan 0.4 hadi 0.5, lakini umbali huo kwa gari la nishati mpya ni Yuan 0.1 tu."
Mbali na gharama ya matumizi ya mafuta, naibu meneja mkuu wa kampuni ya nishati mpya ya Kundi la Magari la Beijing Bw. Zhang Yong pia ametuelezea ruzuku za kununua magari ya nishati mpya.
"Serikali imetoa ruzuku kwa wateja wanaonunua magari ya nishati mpya. Kwa mfano, bei ya gari letu jipya aina ya EU260 sokoni ni Yuan laki 2.4 hadi 2.5, lakini baada ya kupunguzwa kutokana na ruzuku inayotolewa na serikali, bei yake inafikia Yuan laki 1.4. Pia magari yanayotumia umeme yanasamehewa kodi ya ununuzi." 


Ingawa magari ya nishati mpya yanazidi kukubalika na wateja kutokana na bei nafuu na gharama ndogo ya kuyatumia, lakini wateja wengi zaidi bado wanataka kusubiri na kuangalia. Umbali ambao magari ya nishati mpya yanaweza kwenda baada ya kuchajiwa na upatikanaji wa vifaa vya kuchaji ni sababu zinazowafanya wateja wengi kusita.
Bw. Yang ambaye ni mtu anayependa kujaribu mambo mapya pia ana wasiwasi na magari ya nishati mpya, akieleza adha iliyomkuta mwenzake anayetumia gari kama hilo.
"Hivi karibuni, mfanyakazi mwenzangu alikuwa anampeleka mtoto wake mgonjwa hospitali, lakini kutokana na kukosa umeme, gari lake lilisimama umbali wa kilomita mbili kutoka nyumbani kwake, hivyo alilazimika kurudi nyumbani kuchukua gari linalotumia mafuta. Jambo kama hilo kweli linasumbua." 

Bw. Yang ameongeza kuwa kuchaji betri ya gari pia ni jambo linalomsumbua, kwani vifaa vya kuchaji magari yanayotumia nishati mpya ni vichache mjini ingawaje aliponunua gari, kampuni ya magari ilimwekea kifaa kama hicho katika eneo anakoishi.
Hata hivyo huenda mpango wa maendeleo ya miaka mitano ijayo wa China utakaotolewa mwaka huu utaweza kumsaidia Bw. Wang kutatua ugumu wa kuchaji beteri. Pendekezo kuhusu mpango huo limeainisha kueneza magari ya nishati mpya, na kuinua kiwango cha utengenezaji wa magari ya umeme.
Naibu meneja mkuu wa kampuni ya nishati mpya ya Kundi la Magari la Beijing Bw. Zhang Yong amesema, uungaji mkono wa serikali ni fursa kwa sekta ya magari ya China kufanyiwa mageuzi na kupata maendeleo. 



"Kwa upande wa magari yanayoendeshwa kwa mafuta, China bado iko nyuma kiteknolojia na kichapa ikilinganishwa na nchi nyingine zenye nguvu katika utengenezaji wa magari. Lakini katika sekta ya nishati mpya, haswa magari yanayotumia umeme pekee, huenda tuna fursa ya kuzipiku nchi hizo. Serikali ya China imetoa uungaji mkono mkubwa kwa sekta ya magari ya nishati mpya, na makampuni mbalimbali ya China yanatarajia kutumia vizuri fursa hiyo. Wito wa kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa hewa chafu pamoja na shinikizo la kimazingira vimehimiza makampuni ya magari ya China kujiingiza kwenye sekta ya magari ya nishati mpya, na kusaidia kuharakisha maendeleo ya sekta hiyo nzima." 

Bw. Zhang amesema kampuni yake pia imetumia fursa za kimaendeleo zinazohamasishwa na mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano kwa kuchukua mtazamo wa kuangalia mbele na kuweka mpango wake wa miaka mitano ijayo.
"Lengo letu la kimkakati ni kufanya mauzo ya magari yafikie laki tano ifikapo mwaka 2020, na kuchukua nafasi za mbele nchini China na hata duniani. Pia tutajenga kituo cha uvumbuzi wa kisayansi wa magari ya nishati mpya chenye ushawishi wa kimataifa, kufanya ushirikiano na vyuo vikuu maarufu vya kimataifa na makampuni yenye teknolojia ya hali ya juu, na kuinua zaidi uwezo wa usanifu na teknolojia kwa kampuni yetu." 

  References and useful resources:  
>>China Daily News 
 
>>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post