Header ads

Header ads
» »Unlabelled » Jinsi ya kufahamu kama simu unayotumia ni Feki au Orijino, kabla haijafungiwa


 
Mambo vipi rafiki?. Je umeshapata au kusikia taarifa ya kufungwa kwa Simu feki, zilizoharibika, au kupotea ifikapo Juni- 2016 na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Nimekuwekea maelezo ya jinsi ya kutambua kama simu yako ni feki au Laa na njia za kufuata endapo utatambua kifaa chako ni feki kabla ya siku husika haijafika.
Vifaa vya mawasiliano vya mkononi – hususan simu za kiganjani na vifaa vya mawasiliano vya kiganjani (tablets) – vina namba maalum inayovitambulisha. Namba hiyo inajulikana kama IMEI ambacho ni kifupi cha International Mobile Equipment Identity.
Kifungu cha 84 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010 kinataka kuwepo kwa mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi. Rajisi hii inajulikana kwa kiingereza kama Central Equipment Identification Register, kwa kifupi CEIR. Sheria inataka rajisi hiyo ihifadhiwe na kuendeshwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Aidha Kanuni za mwaka 2011 za EPOCA kuhusu mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi inawataka watoa huduma wa mawasiliano yanayotumia vifaa vya mkononi kuweka mfumo wa kudumu wa kumbukumbu za namba tambulishi (Equipment Identity Register – EIR) za vifaa vya mkononi vinavyotumika kwenye mitandao yao.
Mfumo huu wa kielektroniki ambao utahifadhi kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi una lengo la kufuatilia namba tambulishi za vifaa vinavyoibiwa, kuharibika, kupotea au ambavyo havikidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano.
Vifaa vyote vya mawasiliano vya mkononi ambavyo vimeibiwa, vimeharibika, kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano havitaweza kufanya kazi kwenye mitandao ya mawasiliano kutumia vifaa vya mkononi. ifikapo mwezi Juni mwaka 2016 kwa mjibu wa Taarifa zilizosamba.
 
Je utaitambua vipi kama Simu yako ni feki au orijino kabla ujafungiwa?
Zifuatazo ni hatua unazoweza kuzitumia kuangalia kama simu yako ni fake, hakuna mahitaji makubwa kufanya hili ila tu unahitaji simu yako unayoitumia na unayotaka kuiangalia. Jinsi ya kuangalia IMEI namba Andika *#06# kisha bonyeza kitufe cha kupiga Baada ya hapo simu yako itakuletea IMEI namba ambapo kama simu yako au kifaa chako kina laini mbili basi kutakuwa na IMEI namba mbili Namba hii pia unaweza kuipata katika boksi la simu ama nyuma ya ya simu hiyo baada ya kutoa betri, utaijua kwa kuwa huwa ni tarakimu 15. Nakili namba hizo pembeni. 

Mfano wa IMEI namba iliyopatikana kwa kupiga *#06# 
Baada ya kuangalia kifaa kama ni feki ama halali Iandike ile namba uliyo nakili katika hatua iliyopita katika sehemu ya kuandikia ujumbe (SMS) Utume ujumbe huo kwenda namba 15090 Baada ya kutuma meseji hiyo utaangaliziwa je hiyo IMEI namba ni ya simu ya aina gani na nani mtengenezaji wa simu hiyo.
Subiri majibu (haitachukua muda mrefu) Ujumbe huo ukija unakuwa na maelezo ya kampuni iliyotengeneza simu hiyo pamoja na jina la simu hiyo. 
         
Mfano wa ujumbe unarudishwa baada ya kutuma IMEI namba Jinsi ya kujua kama simu yako ni feki 

 Kama jina la mtengenezaji wa simu yako pamoja na aina ya simu yako (Uliyo jibiwa baada ya kutuma IMEI namba) haviendani na majina ya simu yako (ambayo yameandikwa katika simu yako) basi ujue simu yako inamashaka na ni vyema kumuuliza muuzaji wako juu ya hilo. 

Kama majina yaliyorudi hayaendani na majina yaliyoandikwa katika simu yako basi upo katika kundi lenye uwezekano wa kuwa na matatizo, Nakushauli ufuate utaratibu na kuibadilisha ama kuacha kuitumia simu hiyo kabla ya mwezi Juni. Kwanini TCRA wanataka tubadilishe simu Vyombo vya usalama vinaweza kukamata wahalifu wa kutumia mitandao ya simu kwa msaada wa IMEI namba hivyo mtu akiwa anatumia simu ambayo haina au ina IMEI namba ambayo sio sahihi anazuia utendaji kazi wa taasisi za usalama hivyo wao kama mamlaka wanatakiwa kuhakikisha kila mtu anatumia simu yenye IMEI namba sahihi.

>>>Tafadhali Click link zifuhatazo kuhungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM  

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post