Kampuni kubwa ya teknolojia ya
Google imetangaza kuchukuwa uamuzi wa kuunda simu za Nexus pasi na
kushirikiana na kampuni nyingine.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa
na kampuni hiyo, simu za Nexus zilizokuwa zikiundwa na Motorola na LG,
sasa zitaundwa na Google pekee.
Kufuatia uamuzi huo, kampuni ya
Google inatarajiwa kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya simu na kuleta
upinzani kwa kampuni maarufu kama vile Apple na Samsung.