Header ads

Header ads
» » Historia ya Simu ya Kwanza ya mkononi Kutumika Duniani


Zaidi ya miaka 42 iliyopita simu ya kwanza ilipigwa kutumia simu ya mkononi, simu hiyo ya kwanza ya mkononi ilitengenezwa na kampuni ya Motorola. Ilikuwa mwezi wa 4 tarehe 3 mwaka 1973 walijaribu kupiga simu kwa kutumia simu hiyo ya kwanza ya mkononi iliyokuwa inafahamika kwa jina la Motorola DynaTAC. Mfanyakazi wa Motorola aitwaye Marty Cooper alitumia simu ya mkononi kupiga simu kwenda ofisi yao (kwenye simu ya mezani), ilipoita na kupokelewa alisema, “Napiga simu kutaka kufahamu kama nasikika vizuri upande huo.”
Cell Phone Inventor Dr. Martin Cooper
Bwana Martin Cooper akishikilia Motorola DynaTAC kushoto kwake na simu yake nyingine aliyokuwa anatumia, picha hii ni ya mwaka 2009.
Simu hii ilikuja kuingia sokoni mwaka 1983 baada ya muda kidogo ikitumia jina la Motorola DynaTAC 8000x na hii ndiyo simu ya kwanza ya mkononi kuingia sokoni na watu kuweza kununua. Na ilikuwa inauzika kwa bei ya juu sana,
dola 3995 za kimarekani za wakati huo, ambayo ni si chini ya Tsh 8,000,000 za kitanzania. Mafanikio ya simu hii ilifanya yatoke matoleo mengine kadhaa ya maboresho zaidi,
Fahamu sifa za Motorola DynaTAC 8000x Ilikuwa inatumia teknolojia ya analogia hivyo haikuwa na uwezo wa kuwekwa laini, teknolojia ilikuwa haijafikia huku. Ilikuwa na uzito wa kilogramu 1.1 ukilinganisha siku hizi simu nyingi zinakuwaga na uzito wa gramu 100 hadi 150 (Kumbuka kilogramu 1 = gramu 1000) Ilikuwa na urefu wa sentimita 33 kwa 8.89 na kawembamba ka sentimita 4.4. Kioo (display) chake kilikuwa kiduchu, cha kuandika mstari mmoja tuu. Iliitaji kuchajiwa kwa muda wa masaa 10 kutoka kutokuwa na chaji kabisa hadi kujaa kabisa Na ata baada ya kuchaji kwa muda wa masaa 10 muda wa maongezi wa takribani dakika 30 tuu ungemaliza chaji hiyo. Mlinganisho rahisi wa ukubwa wa simu hii na zingine za kisasa.

References and useful resources:

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post