Header ads

Header ads
» » Watumiaji wa Facebook wataweza kuweka video kwenye sehemu za Profile picha zao

 

Mtandao mkubwa wa jamii wa Facebook unaounganisha mamilioni ya watu kote duniani, umeleta maboresho kwenye kurasa za Profile za watumiaji wake.
Kulingana na maboresho hayo, watumiaji sasa watapata fursa ya kuweka video pia kwenye sehemu ya picha za Profile katika kurasa zao Facebook.
Watumiaji wa Facebook wanaweza kujirekodi video fupi za maelezo binafsi na wasifu wao ili kujitambulisha kwa watumiaji wengine wanaoingia kwenye kurasa za Profile zao.
Facebook imetangaza kwamba maboresho hayo yatafanyiwa majaribio katika nchi za Uingereza na Marekani kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa watumiaji wa nchi nyinginezo.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post