Header ads

Header ads
» » Hawa ndio Wadukuzi (Hackers) maarufu zaidi duniani

Wadukuzi maarufu zaidi duniani: Robert Tappan Morris

1. Robert Tappan Morris

Morris alipata umarufu kwa kuunda “worm” ya kwanza ya kompyuta katika mwaka wa 1988

Robert Tappan Morris alizaliwa tarehe 8 Novemba katika mwaka wa 1965. Alipata mafunzo kutoka chuo kikuu cha Harvard na aliwahi kufanya kazi kama mwanasayansi mkuu wa kompyuta katika shirika la Bell.
Katika mwaka wa 1988 alipata umaarufu mkubwa jambo kwa programu hatari aliyounda. Programu hiyo iliyokuwa “worm” ya kwanza kuundwa ilikuwa ikisemekana kutathmini kasi ya mtandao wa intaneti bali kinyume na hayo programu hiyo ilikuwa ikikata mawasiliano ya intaneti katika kompyuta.
Je aliwahi kuadhibiwa?
Morris alipewa kifungo cha miaka 3, masaa 400 ya huduma ya jamii na pia faini ya dola 10,500.
Hivi sasa Morris ni mkufunzi katika chuo Kikuu cha MIT.

2. Jonathan James 

Wadukuzi maarufu zaidi duniani: Jonathan James Hacker

Jonathan James ndiye mdukuzi wa kwanza kukamatwa akiwa chini ya umri wa miaka 18.

Jonathan alizaliwa tarehe 12 mwezi Desemba mwaka wa 1983. Alipata umaarufu alipohukumiwa kifungo akiwa na umri wa miaka 16 kwa makosa ya udukuzi aliyofanya akiwa na umri wa miaka 15.
Jonathan alidukua mifumo ya kompyuta katika wizara ya Ulinzi ya Marekani. Jonathan pia aliwahi kudukua mfumo wa Kompyuta wa NASA na kuiba programu yenye thamani ya dola milioni 1.7.

Je aliwahi kuadhibiwa?

Jonathan alipatwa na hatia na kupewa kifungo cha miaka 10 bali alibahatika kupunguziwa kifungo hicho hadi miezi 6. Jonathan alipigwa marufuku ya kutumia kompyuta.
Katika mwaka wa 2008 Jonathan alifariki kutokana na jeraha baada ya kujipiga risasi mwenyewe

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post