Kampuni nyingi ziliwahi kuboresha mifumo ya usasishaji kwa ajili ya kukabiliana na Stagefright .
Sasa virusi vipya vya Stagefright 2.0 vimeboreshwa na kuwa tishio kubwa vifaa vinavyoendeshwa kwa mfumo wa Android.
Baadhi ya mbinu zinazotumiwa na Stagefright 2.0 kuvamia vifaa vya Android ni;
-Kuchochea watumiaji kuzuru tovuti flani zenye virusi
-Kulaghai watumiaji kwa ujumbe na program za kujikinga zilizobeba virusi
-Kulaghai watumiaji katika programu za kucheza muziki na video zenye virusi.
Kampuni ya Google inasubiriwa kuchukuwa hatua kali na kuifunga programu hiyo.