Akihutubia kwenye mkutano wa maendeleo ya Afrika, Bi. Jeannette Kagame alihimiza wasichana wa Kiafrika kuzingatia masomo ya kompyuta ili kuchangia maendeleo ya teknolojia barani Afrika.
Bi. Jeannette Kagame alibainisha kuachwa nyuma kwa wasichana na wanawake wengi wa Kiafrika kutokana na ukosefu wa elimu ya ICT.
Rwanda imekuwa ikifanya kampeni za kuboresha taaluma katika nyanja za sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati.
Mnamo mwezi Agosti, Rwanda iliandaa kongamano maalum la wiki tatu ambapo wanafunzi wa kike 120 kutoka Ethiopia, Ghana, Kenya, Nigeria, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda na Marekani walihudhuria.