Header ads

Header ads
» » Hatimae Huduma ya WhatsApp Web yafikia watumiaji wa simu za iPhone

 Habari njema kwa watumiaji wa iPhone
Huduma ya mawasiliano ya WhatsApp Web iliyokuwa ikitumika kwenye simu za Android, Windows Phone na Black Berry sasa pia imeingizwa kwenye simu za iPhone.
Watumiaji wa simu za iPhone wataweza kuunga programu zao za WhatsApp kwenye tarakilishi kwa kutumia huduma hiyo ya WhatsApp Web.
Ili kuweza kuanza kutumia huduma ya WhatsApp Web, watumiaji wa simu za iPhone wanatakiwa kuingia kwenye sehemu ya kitufe cha mipangilio na kuichagua katika programu zao za WhatsApp.
Wakati huo huo, watapaswa kufungua tovuti ya web.whatsapp.com kwenye tarakilishi zao na kuunganisha simu kwa kutumia kisimbuzi cha kodi ya QR.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post