Matumizi mabaya ya simu ambayo yamekuwa yakifanywa na
watoto wao kwa ajili ya kufanikisha michongo isiyo na tija, kampuni moja ya teknolojia iligundua mfumo
unaowawezesha wazazi kufuatilia mwendendo wa simu za watoto wao.
Mfumo huo unaojulikana kwa jina la
Belimo, ambao unaweza kufanya kazi kupitia mtandao wa
Vodafone, unatoa fursa kwa wazazi kudhibiti muda wa watoto wao kuweza
kuwa hewani, kutuma ujumbe mfupi wa maandishi au hata kupiga simu.
Tofauti na mifumo mingine inayojulikana
kwa lugha ya kiingereza kama Application, mfumo huu umetengenezwa katika
namna ambayo mtoto anayedhibitiwa hawezi kuukataa kwa namna yoyote ile
kwani anayekuwa na uwezo wa kuuendesha na kuuamuru ni mzazi anayeamua
kuutumia.
Tayari mfumo huu umeshapata umaarufu baada ya kutumika ambapo asasi moja ya nchini Uingereza
yenye kujihusisha na masuala ya uzazi na malezi, imeweka bayana mtazamo
wake juu ya kuukubali mfumo huu
Chini ya mfumo huu, mzazi anaweza
kununua kifurushi ambacho kinajumuisha kadi ya simu ya kawaida tu kama
zilivyo zinazotumika kwenye simu hivi sasa, lakini ikiwa imeunganishwa
kwenye mfumo huo, na huduma hiyo ni ya kulipia kwa kadiri mtumiaji
anavyopenda kuendelea kuitumia.
“Mfumo huu unawezesha wazazi kudhibiti
kwa mfano, namba zipi ambazo hawapendi ziwe zinawasiliana na mtoto wao,
muda wa kupiga simu, kutuma ujumbe na huduma zingine za simu. Lakini
pia, wazazi watakuwa na uwezo wa kusoma ujumbe mfupi wa maneno ulioko
kwenye simu za watoto wao, bila kuwa na simu za watoto hao” alisema
msemaji mmoja wa kampuni iliyoandaa mfumo huo.
Hatua hii imekuja ikiwa ni katika zama
ambazo taasisi kadhaa za kiutafiti zimetanabaisha kuwa, watoto hasa wa
kike barani Ulaya, wamekuwa katika shinikizo la kutuma kwa njia
mbalimbali, mambo yenye kuhusu maisha yao ya kimapenzi, jambo ambalo
limekuwa likiwakwaza wazazi wao huku maadili pia yakizidi kupotea.
Chanzo: newstimes.com