Mkurugenzi mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg amenunua nyumba 4 kwa ajili ya kuzibomoa na kujenga upya katika eneo la Palo Alto lililoko mjini California.
Zuckerberg alinunua nyumba hizo 4 kwa bei ya fedha dola milioni 30.
Hizo rangi nyekundu ndizo nyumba alizonunua Zuckerberg
Ramani
ya ujenzi wa nyumba mpya katika eneo lililokuwa na nyumba alizonunua
Zuckerberg iliwasilishwa kwa idara ya mipango na mazingiria wiki
iliyopita.Nyumba hizo 4 alizonunua Zuckerberg, 2 ni za ghorofa moja na nyingine 2 ni za ghorofa mbili.
Kwa mujibu wa ramani hiyo, Zuckerberg atajenga nyumba 3 za ghorofa moja na nyingine 1 ya ghorofa mbili.
Picha za Nyumba hizo: Picha na CNN website
Chanzo: Cnn.com