Header ads

Header ads
» » Wanafunzi Jiepusheni na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii

Matukio mengi yanaendelea kutokea yakiusishwa na Wanafunzi kutumia vibaya Mitandao ya Kijamii. Hii ni pamoja na Wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Kampala(KIU) kampasi ya Dar es Salaam, kufifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kujibu shitaka la kusambaza picha za kumkashifu Rais John Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Washitakiwa hao ni Amenitha Kongo(19), Maria Tweve (20), Agnes Gabriel(21) na Anne Mwansasu(21), ambapo walipandishwa mahakamani na kusomewa shtaka linalowakabili mbele ya Hakimu Mkazi Catherine Kiyoja.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanadaiwa kuchapisha picha ambazo zinaonyesha Rais Magufuli akiwa amevaa hijabu kama mwanamke wa Kiislamu na kuzisambaza kwenye mtandao huo wa WhatsApp, huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Washtakiwa wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kitimiza masharti ya dhamana.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post