Teknolojia imetuondoa katika mazingira yaliyokuwa yakituzunguka na kutupeleka katika mazingira ambayo si halisi, tuna marafiki wengi wa mitandaoni kuliko marafiki tulionao shule au kazini. Tunatumia muda mwingi katika smartphones zetu kuliko kuongea na wale wanaotuzunguka.
Miaka ya zamani, kabla ya teknolojia kuitawala dunia watu walikuwa
wakienda sehemu wasizozijua kwa kuelekezwa na mtu mwingine au kutumia
ramani iliyopo katika karatasi. Tofauti na siku hizi, hatujui hata
kusoma ramani, tunapata shida kujua alama za barabarani na hatuna muda
wa kusoma maelezo yaliyopo njiani na katika majengo. Unaenda sehemu
usiyofahamu? Sawa! Google Maps itakuelekeza kuanzia ulipo na upite wapi
mpaka kufika unapohitaji kwenda, rahisi sana eeh!
Smartphones na wearable devices kama smartwatches na fitness trackers
zina uwezo wa kutuambia tumetembea hatua ngapi kwa siku, tumepunguza
uzito kiasi gani na mambo mengine mengi mno. Jokofu(fridge) linaweza
tuma taarifa katika smartphone yako kukujulisha ni mahitaji yapi
yanakaribia kuisha ndani yake, huna haja tena ya kulifungua na kukagua
na kupoteza muda. Haya yote ni faida kubwa sana kwetu kwa sababu huokoa
muda na kufanya maisha kuwa rahisi mno.
Fridge ya Samsung itumiayo Android OS. |
Ingawa tuna apps lukuki katika smartphone zetu zinazotuelekeza jinsi ya
kula mlo wenye kuleta afya, njia bora za kufanya mazoezi na kujipa
mapumziko, jinsi ya kupika chakula bora, namna ya kupangilia muda kwa
ufanisi zaidi, jinsi ya kuendesha gari kwa umakini na kufata alama za
barabarani na mengine mengi. Lakini afya zetu si nzuri ukilinganisha na
watu wa zamani, hatujui namna ya kupangilia muda wetu, ni madereva
wabaya na wenye vurugu mno, maisha yetu yana msongo wa mawazo kila
kukicha, tofauti kabisa na watu wa miaka ya zamani.
Teknolojia imefanya mengi mno katika kumletea mwanadamu maendeleo,
ukiangalia maisha ya watu wengi yanaokolewa mahospitalini kutokana ma
matumizi ya vifaa vilivyo na teknolojia ya hali ya juu, si shida tena
kufanya mawasiliano kokote duniani, uzalishaji umezidi kuongezeka na
faida nyingine nyingi nyingi. Lakini, teknolojia hii inatufanya kupoteza
maarifa ya kujua kufanya vitu vingi vya msingi(basic things). Kwa nini
ufue kwa mkono? Mashine iko pale! huhitaji kujua muelekeo wa
unapokwenda, GPS navigator ipo katika gari yako kwa ajili ya kazi hiyo.
Changamoto ni kubwa sana katika teknolojia!