Header ads

Header ads
» » Ngoma amfunika okwi...Apewa Jumba na Gari la Kifalme...Mshahara Kufuru!!



YANGA inaendelea kuonyesha jeuri ‘town’ baada ya ofa nono ya mshahara waliyompa mshambuliaji wao mpya, Mzimbabwe, Donald Ngoma unaomfanya kuwa mchezaji pekee wa Ligi Kuu Bara kwa sasa anayepokea kitita kirefu zaidi mwisho wa mwezi.

Ngoma ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo akitokea Platinum FC ya Zimbabwe, ameingia kandarasi hiyo kwa makubaliano ya kupokea mshahara wa dola za kimarekani 4,000 kwa mwezi ambazo ni zaidi ya Sh milioni 7.9.



Mshahara huo unamfanya Ngoma kuwa kinara wa kuchukua mpunga mrefu zaidi huku akiwazidi wachezaji wengine ghali wa ligi ya Bongo waliokuwa wakitamba awali, wakiwemo Mganda, Emmanuel Okwi anayeongoza kwa upande wa wachezaji wa Simba kwa kuchukua dola 3,000 ambazo ni sawa na Sh 6,000,000.

Kiasi cha pesa anachochota Ngoma pia kimepindua ufalme wa kiungo Mbrazili wa Yanga, Andrey Coutinho na Mnyarwanda Haruna Niyonzima aliyeboreshewa mkataba baada ya hivi karibuni kuongeza mwingine klabuni hapo na kufikia kiasi cha kulipwa Shilingi 7,000,000 kwa mwezi kila mmoja wao.



Fedha hizo pia zinamfanya Ngoma ambaye anarejea nchini ndani ya wiki hii kutoka kwao Zimbabwe, kukusanya Sh milioni 96 kwa mwaka mmoja pekee.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga pia zimefafanua kuwa, straika huyo atakaporejea nchini kuanza kazi, atakabidhiwa gari ndogo yenye thamani sawa na yeye kwa ajili ya usafiri wa ndani na mambo mengine.
Kingine kikubwa zaidi ni kuhusiana na ishu ya nyumba ambapo mpaka sasa anatafutiwa kwenye sehemu nzuri na iliyotulia ili aweze kuwa na utulivu katika muda wote atakaokua nchini.

Yote hayo yameelezwa kuwa ni kutokana na kupigania saini ya straika huyo ambaye alikuwa akinyemelewa kimyakimya na matajiri wa DR Congo, TP Mazembe na imedaiwa kama Yanga ingezubaa kidogo basi ingekula kwao.

“Kila kitu kimekwenda sawa, wala hakukuwa na tatizo isipokuwa ishu ya kutakiwa na Mazembe nayo ilivuruga kidogo ndiyo maana kukahitajika nguvu ya ziada kwa ajili ya kutuliza mambo na kama unavyoona, ukiachana na mshahara pia akirudi imepita ishu ya kupewa gari na nyumba,” kilisema chanzo hicho.

Ngoma ametua kikosini hapo kwa shinikizo la Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm baada ya kuvutiwa na uwezo wa staa huyo aliouonyesha alipokuwa na Platinum ilipopambana na Yanga katika mechi ya marudiano kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post