Dakika kadhaa kabla kipindi cha mapumziko kaka mkubwa wa Messi, Rodrigo aligongwa na kitu kilichotupwa na mashabiki wa Chile jambo lililopelekea kuondoshwa kwa familia hiyo kutoka eneo la mashabiki.
Messi kwa mara nyingine alishindwa kuiongoza Argentina kufikia taji baada ya kulemewa katika mikwaju ya penalti.
Chile waliandikisha historia kwa kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza.