Kunako
dakika ya 9 kipindi cha pili ama waweza sema dakika ya 56 ya mtanange
wa Simba na Yanga, mganda anaecheza soka la kulipwa nchini Tanzania na
klabu ya Simba yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi katika viunga vya
Kariakoo jijini Dar es Salaam, Emmanuel Okwi ameiandikia Simba bao la
kwanza baada ya kumalizia kazi nzuri ya Ibrahim Hajibu. Mpira
umemalizika na Simba 1 Yanga 0.
Mchezaji wa Yanga Harun Niyozima anapigwa kadi nyekundu.
Wakati huo huo Yanga inampeleka Benchi, Mrisho Ngasa na Simba Ibrahim Hajibu nae akaenda benchi.