Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza
na waandishi wa katika mkutano uliofanyika mchana huu kwenye ukumbi wa
mikutano wa ofini za Wizara hizo,zilizopo kwenye Mtaa wa Samora,Jijini
Dar es salaam.Waziri Muhongo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake
huo,kufuatia shinikizo la muda mrefu la kumtaka afanye hivyo au
awajibishwe, kufuatia mapendekezo ya Bunge lililopita, lililoagiza
serikali kuchukua hatua dhidi yake na wengine kadhaa kufuatia kashfa ya
akaunti ya Tegeta Escrow.Waziri Muhongo akikazia kujiuzulu kwake huko
amesema kuwa yeye sio mla rushwa bali ni mchapa kazi tu na
akilizungumzia swala la akaunti ya Tegeta Escrow ambalo ndilo
lililopelekea kujiuzulu kwake huko,Waziri Muhongo amesema kuwa
sakata hilo lilitawaliwa na mambo makuu manne ambayo aliyataja kuwa ni
Mvutano wa kibiashara,Mvutano wa kisiasa,Mvutano wa uongozi na madaraka
pamoja na Ubinafsi.hivyo ameamua kujiuzulu ili kuiachia Serikali na
Bunge kusitisha malumbano ya sakata la Escrow, akidai inaonekana yeye
ndiyo tatizo.Picha/habari na Othman Michuzi.
Sehemu ya Waandishi wa kutoka vyombo mbali mbali vya habari wakifatilia kwa makini taarifa ya Waziri Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akisisitiza jambo wakati akilizungumzia swala la Akaunti ya Tegeta Escrow ambalo ndilo lililopelekea kujiuzulu kwake huko,mchana wa leo.