Taasisi ya mawasiliano ya habari ya China imekadiria kuwa pato la makampuni ya mtandao wa Internet la China litafikia dola bilioni 178 za kimarekani mwaka huu, na linatarajiwa kufikia dola bilioni 253 za kimarekani mwaka kesho. Kutokana na makadirio hayo, kasi ya ongezeko itakuwa ni zaidi ya asilimia 40. Imefahamika kuwa makampuni ya China yamechukua nafasi nne kati ya makampuni kumi makubwa ya mtandao wa Internet duniani.
Kampuni ya ALIBABA imeshika nafasi ya nne, kampuni ya Tencent imeshika nafasi ya tano, kampuni ya Baidu ikiwa nafasi ya saba na kampuni ya Jingdong imeshika nafasi ya kumi.
Chanzo> topnews.in