HALMASHAURI ya Wilaya Same imeanza kupokea faraja za msaada wa kompyuta mbili kati ya sita zilizofikishwa mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni siku chache baada ya ofisi yao kuungua moto na kutekeza vifaa mbalimbali vya kiofisi.
Kompyuta hizo zilipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick, akiambatana na wakuu wa idara wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na watumishi mbalimbali kutoka kwenye halmashauri za Same na Mwanga.
Mkuu wa
Mkoa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick wa pili kutoka kushoto,
akimkabidhi kompyuta hizo alizopokea kwa Taasisi ya Bayport Financial
Services, Katibu Tawala wake wa Mkoa, Mheshimiwa Aisha Amour.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki katika hafla ya kupokea kompyuta hizo, Mratibu wa
Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa,
alisema wamekabidhi kompyuta hizo, ikiwa ni siku chache baada ya ofisi
za Halmashauri ya Wilaya ya Same kuungua moto.
Alisema
ingawa msaada wao umekuja kabla ya ofisi hizo kuungua moto, lakini
wanaamini kuwa kompyuta hizo zinaweza kupunguza adha ya watumishi wa
umma kufanya kazi kwa wakati mgumu, huku zikilengwa kwa Halmashauri ya
Same, Mwanga na Manispaa ya Moshi.
Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Said Mecky Sadick katikati akizungumza
jambo na Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services,
Mercy Mgongolwa kulia bada ya kukabidhiana kompyuta sita za msaada kwa
Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Said Mecky Sadick kushoto akimkabidhi kompyuta mwakilishi wa Halmashauri ya Same.
“Taasisi yetu inatoa pole kubwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na watumishi wote wa Same, ila tunaamini kwa kiasi kidogo kompyuta tulizotoa zitawafuta machozi wadau wenzetu wa Same na Serikali yote kwa ujumla hapa nchini,” alisema Mercy.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Mecky Sadick, aliwashukuru sana Bayport kwa
msaada wao wa kompyuta na kuwataka waendelee kuwasaidia watumishi wa Same kwa kuongeza idadi ya kompyuta zao.
msaada wao wa kompyuta na kuwataka waendelee kuwasaidia watumishi wa Same kwa kuongeza idadi ya kompyuta zao.
“Tunapokea kompyuta hizi kwa mikono miwili lakini tunawaomba wenztu wa Bayport muongeze idadi ya kompyuta kwa Halmashauri ya Same kwa sababu kule kuna uhitaji mkubwa zaidi baada ya ofisi kuungua moto.
“Ofisi yetu imepata pigo kubwa mno hivyo mtusaidie kwa hilo kwa sababu tunafahamu msaada wenu ni muhimu kwetu na taasisi yenu imekuwa karibu sana na jamii kwa kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii ambayo yana tija kwetu sote,” alisema RC Sadick.
Utaratibu wa utoaji wa kompyuta 205 kwa ofisi za serikali zenye thamani ya Sh Milioni 500 umeanzishwa ili kuwafanya watumishi wa serikali wafanye kazi zao kwa ufanisi ili kuhamasisha masuala ya kimaendeleo hapa nchini.(P.T)