Kwa taarifa yake mtendaji mkuu wa kampuni ya Oracle, Safra Catz
ambaye pia alihudhuria kikao cha mazungumzo kati ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump na wataalam wa teknolojia ya mawasiliano
alisema, kama Trump ataweza kufanyia
kazi mabadiliko kanuni ya kodi, kupunguza udhibiti na kujadili mipango
bora ya biashara, teknolojia nchini Marekani itakuwa imara na ya
ushindani zaidi kuliko ilivyowahi kutokea awali.
Makampuni
maarufu ya kiteknolojia kama vile Apple, facebook na Tesla Motors
yalipata nafasi ya kutangaza vipaumbele vyao kama vile mfumo wa
kubadilisha taarifa kwenda katika kanuni maalum ambayo itadhibiti
kupatikana kwa taarifa kwa mtu ambaye hajaruhusiwa na pia ulinzi wa
maudhui ya watumiaji wake.
Athari za Urais wa Trump katika sekta ya teknolojia na mawasiliano ni
ngumu kutabilika, wakati huo kukiwa na uwezekano wa sekta hiyo kupinga
mipaka yoyote ya kibiashara pamoja na ukomo wa wahamiaji. Makampuni
mengi yanatarajiwa kuunga mkono masuala kadhaa kama vile kupunguzwa kwa
viwango vya kodi kwa makampuni hasa katika faida ambayo inapatikana
kutoka nje ya nchi.
Kwa upande mwingine, kuna uwezekano wa kuwepo
kwa mvutano kati ya Trump na sekta hiyo katika suala la kuthibiti wa
upatikanaji wa taarifa ya ujumbe wa siri unaotumwa kupitia katika
mitandao, na uwezo wa maafisa wa usalama na idara za ujasusi kuweza
kutumia taarifa hizo kwa kutumia vifaa maalum kubaini ujumbe na
kuendesha uchunguzi katika masuala ya usalama wa kitaifa.
Trump
kwa upande wake alisema, uongozi wake utakuwa ukifanya kazi kwa
kushirikiana na sekta binafsi ili kuboresha mazingira ya kibiashara na
kufanya kuwa ya kuvutia kwa makampuni ili kutengeneza nafasi mpya za
kazi nchini Marekani.