TeknoTaarifa inatoa Pongezi za dhati kwa Jeshi la Polisi - Kitengo cha Usalama
Barabarani kwa kutokomeza ajali zisababishwazo na mwendokasi kwa
kuzishughulikia taarifa zinazotumwa na watumiaji wa #Makiniapp.
Ewe mdau,Download Makiniapp ili uweze kuitumia ukiwa
safarini na uweze kutambua pindi dereva anapoendesha kuzidi kikomo cha
mwendokasi cha barabara husika.
Kwa pamoja tunathubutu kutokomeza ajali zisababishwazo na mwendokasi.
Msemaji mkuu wa MakiniApp Irene Kidunda Alisema
"MakiniApp hii ni application ambayo inamuwezesha mtumiaji
kufahamu kiwango halisi cha mwendokasi wakati anaoutumia dereva wakati
wa safari kupitia simu yake‘
‘Ikiwa dereva anatembea kwa mwendokasi usiotakiwa mtumiaji
anaweza kuchukua hiyo taarifa na kuituma katika kikosi cha usalama
barabarani kupitia hiyohiyo simu yake ili askari wamchukulie hatua
dereva huyo"
Aliendelea kusema
"Uzuri wa kuwa na application hii ni kwamba hatakama hutakuwa na mtandao
kwa muda huo bado utakuwa na uwezo wa kurekodi mwendokasi wote na kisha
ukampatia askari polisi utakayemkuta barabarani na bado ikawa na msaada"
MakiniApp imerasimishwa kua application pekee Tanzania
itakayotumika na jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kwa ajili ya
kupokea taarifa za mwendokasi zitakazokua zikitumwa na abiria wa vyombo
vya moto (pikipiki na motokaa) waliotumia MakiniApp ili kuepeusha ajali
zisababishwazo na mwendokasi.
- Taarifa itakusanywa na MakiniApp.
-
Itatumwa kwa namba ya simu ya jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama
barabarani (0682 88 77 22 - ambayo imeunganishwa na mitandao ya kijamii
yaani Whatsapp na Telegram na kufanyiwa kazi mara moja.
Kwa
pamoja tushirikiane kutokomeza ajali za mwendokasi kwa kuhimiza
matumizi ya MakiniApp ili tupeleke taarifa za mwendokasi zilizo na
vithibitisho.