Header ads

Header ads
» » Naijeria Taifa Linaloongoza kwa Matumizi ya Facebook Barani Afrika



Licha ya Nigeria kudorora kiuchumi lakini imeongoza kwa kuwa na watumiaji takribani milioni 16 wa Facebook. Kitendo cha Nigeria kuongoza kwa kuwa na watumiji wengi wa Facebook inamaanisha kuwa matumizi ya intaneti ni makubwa nchini humo. Mwaka jana Afrika Kusini iliongoza kwa kuwa na watumiaji milioni 12 wa Facebook ikifuatiwa na Kenya (mil. 4.5). Nigeria inawatumiaji wa kila siku wa Facebook milioni 7.2 huku asilimia 97 kati ya hao wakitumia simu kuingia Facebbok. 
 facebook-users-nigeria
Afrika Kusini kwa Madiba ndio inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaotumia simu kuingia Facebook ikiongoza kwa 34%, Nigeria (27%), Senegal na Kenya wote wakiwa na 15%, wakifuatiwa na Ghana (14%) huku Tanzania (8%). 
 
Facebook yahusika katika kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja Watu wengi hasa nchini Nigeria wameweza kukuza vipato vyao vya kila siku kwa kutumia mtandao wa Facebook kutangaza bidhaa zao wakitumia simu janja kuingia katika mtandao huo na kutangaza biashara zao na kuweza kukuza soko la bidhaa zao ndani na je ya Afrika kwa kutumia Facebook 

Chanzo: thenewsnigeria.com.

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post