Katika kile kinachoonekana kwa Israel kuendelea na mchakato wa kutaka
kuwa karibu na Nchi za Afrika, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Bw. Benjamin Netanyau alikutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya
viongozi wa nchi za Afrika wanaohudhuria
Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Vipaumbele ambavyo Waziri Mkuu amevieleza mbele ya viongozi hao pamoja na
mambo mengine katika maeneo
ya za usalama na teknolojia.
Tanzania ikiwakilishwa na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga ni kati
ya nchi za Afrika zilizoalikwa kuhudhuria
na kushiriki mkutano huo. Dkt Mahiga
anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Akichangia vipaumbele hivyo vya Israel kwa Afrika, Waziri Mahiga amesema usalama na
teknolojia ni mambo muhimu katika
maendeleo ya nchi yoyote ile na hususani zinazoendelea.
“Israel imetambua kuwa usalama na
teknolojia ni maeneo muhimu
ambayo nchi zetu zinaweza kushirikiana. Na sisi Tanzania tungependa kuyatambua maeneo
hayo kwa sababu ni kweli ulinzi na teknolojia ni nyenzo muhimu kwa
maendeleo”. Akasema Balozi Mahinga
Akaeleza kwamba kinachotakiwa kuanzia
baada ya mkutano huo uainishaji wa
namna gani ya kuanza majadiliano iwe kati ya Israel na nchi moja moja ( bilateral )
au kwa katika mfumo wa majadiliano ya kikanda.
Vyovyote vile itakavyokuwa Waziri
Mahiga amesisitiza kwamba,
majadiliano hayo lazima yawe jumuishi, yasiyobagua na yenye manufaa kwa
pande zote mbili. Kauli iliyopigiwa
makofi na washiriki wengine ikiwa ni ishara ya kuiunga mkono.
Chanzo: israelnationalnews.com