Rais wa Uturuki Erdogan aweka rekodi ya wafuasi wa Twitter
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameweka rekodi kwenye mtandao wa jamii wa Twitter kwa idadi kubwa ya wafuasi.
Baadhi ya maelezo yaliyonukuliwa kutoka kwenye hotuba ya Erdogan ya mkutano wa baraza kuu la UN nchini Marekani yalisambazwa kwenye mtandao wa jamii wa Twitter kwa lugha 4 tofauti.
Maelezo hayo yanayojumuisha suala la wakimbizi wa Syria alilozungumzia kwenye mkutano wa 71 wa baraza kuu la UN yalifikia mamilioni ya watumiaji wa Twitter.
Rais Erdogan alivutia wafuasi wengi kwa ujumbe wake uliosambazwa kwa kutumia hashtag ya #ErdoganSautiYaWanyonge.
Kwa majibu wa takwimu zilizotolewa na mhusika kuu wa akaunti ya Twitter ya Erdogan , Ismail Cesur, maelezo hayo yaliyosambazwa kwa lugha za Kituruki, Kiingereza, Kifaransa na Kiarabu yalisomwa na watumiaji milioni 13,360,000.
Jumbe 12 zilizosambazwa kwa lugha ya Kituruki zilifikia watumiaji 4,780,000.
Ujumbe mmoja pekee wa uliosambazwa pia umeweza kufikia watumiaji zaidi ya milioni.
Chanzo: trt.net.tr/