Nigeria yafahamisha kuwa ina mpango kupeleka mwanaanga angani kuendeleza sekta ya masuala ya anga katika kiwango cha kimataifa mwaka 2030.
Katika hotuba yake mjini Abuja,waziri wa sayansi na teknolojia Ogbonnaya Onu alisema kuwa ni lazima Nigeria kushirika katika masuala la anga kwa madhumuni ya kulinda maslahi ya taifa.
Shirika la anga la Nigeria latarajiwa kufanya ziara ya China mwezi huu kwa lengo la kukutana na washirika wenzao wa China kufanya majadiiliano kuhusu uwekezaji na logistiki za shughuli hiyo ya angani.
Chanzo: CNN News
Mhariri: AbdallahMagana.com